JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, SACP David Misime
YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA
VYOMBO VYA HABARI TAREHE 14/07/2015
Napenda kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa 10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi walitoa taarifa majira ya saa nne asubuhi kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa. Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli.
Askari walithibitisha kuwa ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/= ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka. Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.
Akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St. GASPER walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi. Mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa uchaguzi kati ya makundi mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.
Katika tukio hili na uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.
Aidha imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake.
Aidha tarehe 10.07.2015 majira ya saa 21:00 eneo la Railway Dodoma tulifanikiwa kuwakamata:-
1. HERERIMANA METHODE, MIAKA 21.
2. HATUNGIMANA ALEXIS, MIAKA 20.
3. NIYONGABO JUSTIN, MIAKA 20.
4. NTETURUYE ONESPHORE MIAKA 21.
5. BIKORIMANA LEVIS, MIAKA 21 wote ni Wakazi wa Mabanda Burundi kwa kosa la kuingia nchini na kuishi nchini bila kibali.
Watuhumiwa hawa walikuwa wanasafiri na treni kuelekea Dar es Salaam na walipofika Dodoma Askari wanaosindikiza treni waliwashtukia na walipowakamata na kuwahoji walijieleza kuwa ni raia wa Burundi.
Tunaomba ushirikiano wa wananchi pale wanapoona watu ambao siyo raia wasiwakaribishe bali watoe taarifa kwa vyombo vya dola waweze kuhojiwa kwani hata kama waliingia Nchini na kuhifadhiwa katika makambi yaliyopo Nchini hawaruhusiwi kutoka kwenda mbali na kambi zao bila kuwa na kibali maalum.
5 comments:
Thank God wamemrudishia pesa zake. Wabongo nooooooma!
Mambo ndio hayo ya kufunika funika makosa ya rushwa hapa nchini sasa hapa nani ndio mwongo.Hawa watu mkiendelea kuwalea hii nchi mtashidwa kuongoza na kugeuzwa vibaraka, maana hawa watu watakuwa na nguvu kubwa kuliko serikali na kuwapangia maamuzi.Mfano kuwachagulia viongozi, kumwondoa kiongozi yoyote ambaye hawata kubaliana nae, kushidwa kuwachukulia hatua zozote za kiserikali ktk makosa makubwa na madogo nk. Mimi hapa kwa mtazamo wangu hawa watu wamesha shika viongozi kazaa wakubwa ktk serilikali yetu pia wanabeba sili kubwa kwa baazi za viongozi wakubwa hapa nchini,ndio maana hatuwa za kisheria zinashindikana. Rudini nyuma na kusikiliza hotuba za mwalimu nyerere kuhusu rushwa, pia kuhusu yule mgiliki halie mweka ndani kwa kutamba tu kuwa serikali yote kaweka mkononi.Huu ulikuwa wosia wetu kwa serikali kuhusu rushwa.
Mbona hizo za Escrow mmeshindwa kuzipata?
Huu uwongo wa mchana kweupee
Hii ulikuwa ujsnja kupnyesha mtia ia mmoja alikuwa anataka kununua upngozi. Msitidanganye ng'oooo
Uthibitisho utapatikana vipi mbele ya fedha na rushwa nje nje mpaka kwenye uchaguzi wa viongozi mkubwa kama hivi.Hivi tuseme huyu jamaa kama angekamatwa wakati wa mwalimu nyerere si pange nuka mpaka basi.ila kwa sasa issue hii itatoweka kama vile hatuna serikali.
This is nothinG but bul----lSHIT
Post a Comment