Advertisements

Friday, July 17, 2015

JOYCE KIRIA ATOA KAULI KUHUSU KUKAMATWA KWA BLOGGER MANGE KIMAMBI ‪


‪#TAHADHARI‬! Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Polisi, Tanzania Human Rights Defenders, Tawla, Wlac, Legal Human Right Center, Wildaf, Tume ya Haki za Binadam, Tamwa, Tgnp, Wananzania wote wapenda Maendeleo ya Halali, msaidieni huyu Mwanaharakati aliyethubutu Kujitosa mithili ya Swala katikati ya msitu ulojaa Simba wenye njaa, Mpiganaji wa kweli aliyejaaliwa Kipawa cha kusema bila kumumunya, ambae amejitokeza kupigania Haki za Binadamu kwa kupiga vita Madawa ya kulevya nchini mwetu!!
Kiukweli @mangekimambi_ Amejitosa upande ambao wengi wetu tunaojiita "Wanaharakati" tumeufumbia macho na tunaogopaaaaa kuwanyooshea vidole wanaohusika kwenye mtandao huo �� Ila huyu Bi @mangekimambi_ Ni mtanzania pekee alieamua kujitoa Sadaka kwa ajili ya Watanzania wenzake hususan vijana wanaoangamia kwa kubwia unga au madawa ya kulevya kila kukicha....
Huyu @mangekimambi_ naona ana uthubutu wa hali ya juu mno katika kukemea maswala mbalimbali kwa maslahi ya wengi hasa Taifa likiwepo la madawa ya Kulevya, na hivyo kuhatarisha uhai wake. Kwa sasa ametangaza kutishiwa Uhai kwenye accont yake ya Insta kwamba kashikiwa BASTOLA jambo ambalo halipaswi kufumbiwa macho kabisa...

Kama kweli tunaipenda nchi yetu basi ni wakati wa kuwalinda Wanaharakati wanaojitokeza kuokoa kizazi cha vijana na Taifa hasa pale wanapojaribu kukemea uovu na kukumbwa na changamoto kubwa kama hiyo ya kutishiwa kuondolewa Uhai wao... Tusisubiri mtu auliwe ndo tuanze kutoa salam za pole bali tuchukue Tahadhari mapema...

Binafsi Nikijaribu kuvaa viatu vya kina RayC, Banza, na wengine wengi nadata na nazidi kukuombea Bi @mangekimambi_ Mungu akulinde kwenye hayo Mapambano maana yeye pekee ndo Mtetezi na Mtenda Haki Milele...
Nimeumizwa sanaaaaaa ila ndo ivo nchi hii tunawatukuza wanaopata pesa kwa kuangamiza watu wengine

No comments: