Kati ya mambo ninayomkubali zaidi Dr Slaa ni KUMBUKUMBU.
Jamaa ana kumbukumbu sana.
Na nahisi hapo anamuangalia Lowassa na kukumbuka yote aliyowahi kusema juu yake.
Afikirie "uchafu" wote waliosema Lowassa anao, bado aonekane "msafi kuwakilisha chama kuliko yeye"
Ni hapo unapotamani uwe na SELECTIVE AMNESIA
Sijui kuna sauti ngapi kichwani mwake sasa?
Na sijui kama kuna inayomuasa kufanya "maamuzi magumu"?:
SOURCE.:.MUBELWA BANDIO
SOURCE.:.MUBELWA BANDIO

11 comments:
Mimi si mwanasiasa lakini ni mwananchi mpenda nchi yangu. Naipenda Tanzania maana ndiyo nchi yangu.
Masikitiko yangu makubwa ni jinsi wanasiasa wetu wanavyotupelekesha kwa malumbano yao kila kukicha, huyu kafanya hiki huyu leo ni fisadi, leo huyu anarudi kundini. Kama mtu anarudi kundini kwa mtazamo wa dini ya Kikirsto ni kwamba alitenda dhambi. Kinachonishangaza mimi leo ni kwamba Lowasa anataka kutuamba ukweli gani wakati huu baada ya kunyofolowa kwenye harakati za kuingia ikulu kama rais. Swali langu ni kwamba kama kweli Lowasa alikuwa safi na mkweli akimwogopa Mungu kwanini hakusema ukweli wakati ule wa tukio, akakaa kimya? Hivi kweli hamuoni aibu CDM kutudanganya leo ya kwamba Lowasa ni msafi, huku wakati uliopita alikuwa fisadi? Je kama CCM ingelipitisha jina lake na kupata kibali cha kugombea uraisi CDM wangelifanyaje? Bila shaka wangelitumia kigezo cha ufisadi wake kwenye kampeni zao ili kumwangusha. Namwomba sana Mheshimiwa Lowasa akumbuke alikotoka. Kiu ya kuwa rais isimfanye kuwa chambo kwa ajili ya waroho wa madaraka.
Watanzania tuweni macho. Naiombea mema nchi yangu, nawaombea Watanzania ili Mungu azidi kutujalia amani. MUNGU IBARIKI TANZANIA
Kwa hiyo unataka kutuaminisha tatizo la uchafu wa CCM ni Lowassa. Akiondoka basi matatizo ya ufisadi yameisha? Tatizo ni chama kilicho madarakani kina mfumo umeoza hivyo kuwa chaka la maovu. Tumekuwa tunaweka watu wapya serikalini lakini hamna different results. Fumua mfumo mzima na kujipanga upya.
Una maoni mazuri nakushukuru kuwa umetangulia kukiri kuwa wewe siyo mwanasiasa. Sasa mpendwa elewa tu Siasa ni mchezo mchafu. Leo kunakuchafuana bila Ukweli. Hata wewe ungesimama leo ukishakuwa tishio kisiasa utachafuliwa pia. Mimi nasema acha tu game ya siasa ichukue mkondo wake. Huenda kuna jambo ambalo Mungu anataka kutuambia Watanzania. Kikubwa sisi Watanzania tuishi tu kwa upendo tusikubali kugawanywa na wanasiasa.
Wandugu. Kitu inaitwa siasa ni mchezo kama wa karata. Siasa inaweza kumchafua na kumsafisha yeyote yule kundini. Na hasa ukija kwenye chama yetu ya CCM utakumbana na mengi sana! Kama kusemwa ni vyama vyote vinamtindo huo na sio CDM pekee! Inapofikia kipindi cha uchaguzi utasikia vijembe sana hivyo ni kiasi vha kuwa watilivu tu..!
Well said mdau hapo juu. Yaani umeongea point tupu, hakuna cha kuongozea.
Well stated!
Siasa za maji taka, wanasiasa wanaoongoza wajinga.Chadema walikuwa wanatafuta umaarufu kwa kumkashfu Lowassa na CCM, LEO AMEKUWA MZURI NA MUADILIFU. IKONGOTI LAUKA IHEMBA. Siasa za Tanzania ni siasa za TUMBO.Hakuna muadilifu hata mmoja, watu woote njaa tu.
ACHENI KUDANGANYWA NA VITENGE, FADHA,MISULI NA T-SHIRT.Tunahitaji viongozi waadilifu wasomi, na viuongozi wanaozungumza sera nzuri sio kutukana na kukashfu kila jema linalofanywa.lowasa anapendwa na watu kwa kuwa ana fedha za kuhonga sasa Chadema wameona ndio wamepata kiongozi.
Kwa wale wanaofuatilia mkongo mzima wa kuelekea uraisi wa Tanzania wakiwa wakweli kwa nafsi zao na kwa waTanzania kwa ujumla wao, wataona kuwa Mhe. Lowasa alianza kuwa na nia ya kugombea urais mapema sana. Alitumia pesa zake nyingi(Kitu cha kutilia mashaka) kuwafadhili au kuyafadhili makundi mbalimbali nje ya utaratibu walijiwekea wenyewe CCM akiwa mwanachama na kiongozi.Hii ina mshiko wa kauli ya Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere aliowahi kuusema kwa kuuliza nanukuu" Hao wanaotaka kuingia Ikulu kwa kutumia pesa walizoazima wakiingia ikulu watalipa hizo pesa kutoka wapi? Ikulu sio nyumba ya biashara, hakuna pesa Ikulu." mwisho wa kunukuu.Sasa tunaposikia urembeshwaji wa Mhe. Lowasa ni kwa usafi au uchafu wake anakuwa chaguo la kwanza la muundo wa upinzani? Tusisahau kuwa CCM imekumbwa na mtikisiko na yeye ni mtajwa wa mara kadhaa. Chadema wanalielewa hilo vilivyo kwa maana ni wao ambao walilipigia kelele hata Mhe. Lowasa kuenguliwa uwaziri mkuu. Leo wanamwona msafi? Kwangu mimi na mimi tu, hii ni dalili kuwa upinzani unapungukiwa nguvu.Na pia tukumbuke kuwa wengi wa wapinzani wame au walilelewa na Serikali hiyo hiyo wanayotaka kuiondoa madarakani ingawa sijui katika kipindi au vipindi mbalimbali vya mpito kwa kila mmoja wao walijifunza chochote chema kwa Tanzania ambacho ni tofauti ya ndugu yetu Lowasa alichokifanya kuruka vyama kwa tamaa ya kuingia ikulu. Wote hawana cha kumchafulia mgombea kupitia CCM maana hadi sasa yeye amekuwa msafi na mwadilifu kwa Tanzania wote wanalifahamu hilo.Angekuwa Lowasa suala la uadilifu kwa nchi yetu lingekuwa kikwazo kikubwa toka kwa hao hao wanaomkaribisha leo.Mwandishi aliyetangulia amegusia mengi kwa upana wake na ni vizuri waTanzania kwa busara zao wakayaangalia na kuyatumia katika kufanya maamuzi mazito kwa Tanzania yetu.Ahsanteni kwa kuusoma ujumbe wangu huu. Mungu Ibariki Tanzania na Watu wake Wakarimu! JB
Wewe ndugu hujui alikula kiapo cha kulinda "maamuzi yote" ya siri sirikalini?
Wewe ndugu hujui alikula kiapo cha kulinda "maamuzi yote" ya siri sirikalini?
Mdau NY hapo juu busara tupu. Watu wanaulalamikia mfumo kama watu ni wachafu na wezi hata ukileta mfumo kutoka kwa mungu mambo yatakuwa yale yale
Post a Comment