ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 20, 2015

MAJAMBAZI WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI, WAKAMATWA

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa watuhumiwa wa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakishari, leo jijini Dar es Salaam.
 Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Stakishari , jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo stakishari, leo jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh.Milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovamia kituo stakishaari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.
 Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Stakiki zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.
 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za amajambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es salaam 
Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Stakishari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka)

Na Chalila Kibuda.
MAJAMBAZI waliovamia Kituo cha Stakishari jijini Dar es Salaam watatu wauwawa na wawili watiwa mbaroni wakati wakitupiana risasi katika eneo la Tuangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la kukamatwa na kuuawa kwa majambazi hao lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Tuangoma Kigamboni jijini Dar es Salaam, majambazi hao walifanya tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao  inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Tuangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.

Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala, Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga.

Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15) ,Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour( 24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.

Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki  15 walizopora katika kituo cha Stakishari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi kuweka kinyesi juu.

Amesema katika Shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibiwa pamoja na kukuta fedha taslimu Sh.Milioni 170 za kitanzania.

Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kuwa hailipi.
Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibwa wapi, na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nazo.

“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.

Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea  julai 12 majira ya saa nne.

CHANZO: MICHUZI BLOG

5 comments:

Jay said...

Kwa mara ya kwanza maishani mwangu Kamanda Kova na watumishi wako nawavulia kofia kwa kazi safi mliofanya juu ya tukio hili. Inabidi muongeze bidii zaidi kutupa moyo wananchi maana mlizidi kutuumiza na kutuvunja imani dhidi yenu.

Anonymous said...

Hongera jeshi la polisi kwa kazi nzuri.Ushauri kwa jeshi la Polisi;
-jeshi lifungue website ambayo itaweka picha na majina ya wahalifu ili iwe rahisi kuwatambua.Hali ilivyo sasa ni kuwa majambazi hawa wanamove from point A to B ,na wengine pengine tunashare nao Meza kwenye bar bila kujua..

Anonymous said...

ningependa kushauri tu kwamba kila kituo cha polisi kiwe na CCTV camera kwan uwezo tunao wa kufanya hivyo na maeneo yote muhimu kama vile hospitali za rufaa ambazo kila siku tunakamata madaktari feki pia ziwepo CCTV

Anonymous said...

Sasa wawekeni picha ili kila MTU awaone ni watu wabaya sana hakuna haja ya kutuwekea vipicha mpaka tuvae vimani wape mugshot ili siku hats kama wakitoroka zero watu waweze kuwatambua sidhani kama kamanda anawasaidia jamii kwa kushika karatasi ya passport photo wakati anao watu mbaroni weka picha wakiwa mbaroni ili jamii nayo ikae kwa amani kujua kweli kwa uhakika hao watu wako mbaroni

Anonymous said...

nyinyi mko huko unyamwezini hamjuagi kinachoendelea huku zaidi ya kuhabarishwa habari tu.

huu ni usanii na Usanii upo mpaka kwa mapolisi wetu. hawajakamatwa hao majambazi;wewe jiulize watu walio dhamiriya kuingia kituo cha polisi unafikiri ni goigoi wakamatwe kizembe zembe namna hivii.

kama kweli wamekamatwa wawaonyeshe sura zao wawe live tuwaone.
japili bunduki zimechakaa hivyo na kama wiki ziliibiwa,kulikoje?

umewahi kuwaona maaskari wetu wakisika aina za smg kama hizo?

pesa walizo zikamata/na mara nyingi wanapozikamata huwa zinapelekwa wapi?

wacha usanii wa movie hii endelea kwa vile uchaguzi unakaribia basi wacha tu movie endelee tutayaona mengi na kuyasikia mengi katika kipindi hichiiii

tona mjua mheshimiwa kovi toka mbeya.kwa nyinyi huko unyamwezini someni tu vijimambo mitandaoni.