ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 23, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MAONESHO YA 10 YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuashiria kufungua  rasmi Maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam.  Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mvumbuzi wa mashine ya kuchujia maji safi, Dkt. Askwar Hilonga, wakati alipotembelea katika Banda la maonesho la Chuo Kikuu cha Nelson Mandela, katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, Atilio Raphael (kushoto kwake) na William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani waliyoibuni maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.
 :- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha, William Sambera (kulia) kuhusu Kompyuta ya mezani iliyobuniwa maalum kwa ajili ya kufundishia somo la Kompyuta, wakati  Makamu alipotembelea Banda la Chuo hicho katika maonesho ya 10 ya Sayansi ya Teknolojia ya Vyuo vya Elimu ya Juu, nchini yanayoendelea kwenye Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, jijini Dar es Salaam. Maonesho hayo yamefunguliwa rasmi leo.

No comments: