ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 30, 2015

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA KIA-MERERANI, JIJINI ARUSHA

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Mji mdogo wa Mererani, wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani yenye Kilometa 26. Hafla hiyo imefanyika leo Julai 30, 2015.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, na baadhi ya viongozi wakifunua kitambaa kwa pamoja kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, wakati wa hafla fupi iliyofanyika mji mdogo wa Mererani, leo Julai 30, 2015.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na baadhi ya Viongozi,kwa pamoja wakikata utepe kuashiria kuzindua rasmi harakati za ujenzi wa Barabara ya Kilometa 26 ya Kia-Mererani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika mji mdogo wa Mererani leo Julai 30, 2015.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makabila mawili makubwa ya Kimasai baada ya kumvisha vazi hilo.
Dkt. Bilal akiagana na viongozi hao wa kabila la Masai.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu  baada ya kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Julai 30, 2015. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi
  Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
  Magufuli, akikabidhiwa fimbo ya heshima ya kabila la Kimasai.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakicheza sambamba na kinamama wa kabila la Kimasai wakati wakifurahia ngoma ya Kimasai kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, wakifurahia ngoma ya asili kwenye hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia-Mererani, leo Mkoani Manyara
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwashukuru wananchi wa zawadi ya vazi la Kimasai, baada ya kuvishwa wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Barabara ya Kia- Mererani, leo Mkoani Manyara. Picha na OMR

7 comments:

Anonymous said...

Km 26 za barabara zinaleta watu wote hawa, makamu wa rais, waziri wa ujenzi na maelfu ya watu ambao wangekuwa wanafanya kazi badala yake wanalundikana hapo. Kwani hizi kazi haziwezi kufanyika kimya kimya kuliko kugharimu kuwasafirisha makamu wa rais na mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya? ingekuwa km 500 si wangekuwa wanakusanyika kila siku?

Anonymous said...

UKIAMBIWA HUU NI UCHIZI WA CCM watu wanakataa? Miaka yote hii 60 na ushee wanajenga km 26 (maili 13 tuuuu) PESA WALIZOTUMIA KWA USAFIRI NA MALAZI KUJA KUWEKA JIWE LA MSINGI ZINATOSHA KUJENGA KM ZINGINE 26!!

Anonymous said...

Kweli namna hii tutaishia kubaki nyuma kimaendeleo, tutaishia kucheza ngoma badala ya kufanya shughuli za maendeleo only 26 km for all that

Anonymous said...

Amka mdau, this is what we call "SMART POLITICS", wanagonga mlangoni mwa LOWASA!

Anonymous said...

Mdau,huu ni wakati wa uchaguzi,tegemea mengi..

Anonymous said...

Obama angekuwa anaweka mawe ya msingi ya barabara na madaraja Marekani, angekuwa alashinda na kulala site.

Anonymous said...

we mdau wa July 31 (saa 1:44 am) - mimi naita hii ni "CHEAP politics"