Advertisements

Wednesday, July 22, 2015

Mizengwe ndani ya Ukawa


Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa mkutano na viongozi wa umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA). 
Umoja huo wa vyama vinne vya NLD, CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema, ulianza vyema mapema Aprili mwaka jana baada ya kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana na kutokubaliana na mwenendo wa Bunge hilo lililokuwa limepewa dhamana ya kupitisha Katiba Mpya.By Nuzulack Dausen
Ni dhahiri kuwa giza nene limeanza kutawala ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), baada ya tukio la kumtangaza mgombea wao wa urais kuahirishwa mara kadhaa, huku Watanzania wakiwa na hamu ya kumfahamu mwanasiasa huyo anayetarajiwa kuchuana na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli.
Umoja huo wa vyama vinne vya NLD, CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema, ulianza vyema mapema Aprili mwaka jana baada ya kutoka katika Bunge Maalumu la Katiba kutokana na kutokubaliana na mwenendo wa Bunge hilo lililokuwa limepewa dhamana ya kupitisha Katiba Mpya.

‘Ndoa’ hiyo iliyovutia nadharia mpya za kisiasa nchini, ndani ya kipindi kifupi ilikomaa na kufanya viongozi wa vyama hivyo kusaini makubaliano ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kusimamisha mgombea mmoja katika kila nafasi.

Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Desemba mwaka jana, hakukuwa na mvutano mkubwa baina ya vyama hivyo kiasi cha kuonekana tegemeo kubwa kwa sasa la kuiangusha CCM.
Credit:Mwananchi

1 comment:

Anonymous said...

Sasa hii ndo mizengwe? Mmekosa habari nyie watu?