Advertisements

Wednesday, July 22, 2015

YANGA BAADA YA KUGEUZWA MASALO NA GOR MAHIA LEO WAKEUKA MCHARO


Baada ya mchezo wa ufunguzi kugeuzwa chachandu na Gor Mahia kwa kuchapwa 2 kwa 1 leo Yanga wamegeuka mcharo baada ya kuwageuza Telecom ya Djibouti chips mayai 3 na pia wakikosa penati 2. Hili swala la penati limekuwa gonjwa ndani ya miguu ya wachezaji wa timu ya Yanga ukikumbuka hii ni penati ya 3 wanakosa katika michezo miwili, mchezo wa ufunguzi na Gor Mahia walikosa moja na leo wamekosa penati 2 wakosaji wa penati hizo ni Msuva na Tambwe. Nikijana mzarendo aliesajiliwa kutoka Mgambo JKT ndiyo aliewapa furaha wapenzi na wanazi wa Yanga kwa kufunga magoli 2 na 1 likifungwa na mzarendo mwingine aliesajiliwa kutoka timu ya daraja la chini kabisa. Vijana kama hawa ni changamoto tosha kuwa mchezo wa mpira ni kujiongeza tu unaweza kusajili mchezaji kutoka nchi nyingine kwa gharama kubwa lakini akaja kugeuka kichekesho cha mwenye mapengo. Kwangu natoa pongezi kwa vijana hawa Malimi Busungu, na Geofrey Mwashuya wakaze sana kwani uwezo wanao na nafasi ndiyo hii ya kufanya makubwa na kuwaacha wageni waliojazwa manoti mifukoni wakijiwashia taa nyekundu wenyewe.

Mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu akishangilia goli lake leo Taifa
Mchezo unaofata ni Ijumaa na KMKM swali ni Yanga watachomoka ndani ya maafande hawa wa maji ya bahari ya hindi na kuingia kwenye kundi la mzunguko wa pili.

No comments: