ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, July 22, 2015

MOSHI MJINI KUMEKUCHA ! KUELEKEA KURA ZA MAONI !NURU MPYA YA MABADILIKO KATIKA UMMA

Baadhi ya wananchi jimboni Moshi Mjini wamesikika wakisema kuwa katika kuelekea kula katika kura za maoni ,hawezi kukubali kuwa msingi watu wa wafanyibiashara
wanaokimbilia dili la kugombea ubunge,wananchi hao wametililika kwa kudai kuwa
hadi sasa kuna wagombea 11 kwa kupitia tiketi ya CCM, ambao wanawania kupata ridhaa ya wanaCCM jimboni Moshi Mjini,katika wagombea hao wapo pia wafanyibiashara na raia wa kawaida,miongoni mwao yupo mgombea mwenye umri mdogo kuliko wote kijana Daudi Babu Mrindoko ambaye ni mjumbe wa umoja wa vijana UVCCM mkoa Kilimanjaro na pia mwenyekiti wa Umoja wa Wazalendo Tanzania(UWAWATA),inasemekana wakazi wa Moshi Mjini wanamuamini kijana
huyo kuwa ndio JEMBE na NYUNDO yao kwa kuwa si mpenda makuu wala haitaji kuwafanya wapiga kura wake kuwa msingi watu wa biashara.


Wananchi wa jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro mwanzoni mwa mwaka 2015 walianza kumshawishi kijana Daudi Babu Mrindoko kuchukua fomu za kugombea ubunge wa jimbo la Moshi-Mjini,Wananchi jimboni Moshi-Mjini wanaamini kabisa kuwa pendekezo lao la mgombea Daudi Mrindoko ndio funguo pekee ya kumaliza matatizo na ndio funguo ya kuelekea kwenye nuru mpya ya maendeleo jimboni. 
Pendekezo hilo la wananchi wa Moshi Mjini kijana Daudi Mrindoko ambaye ndiye mgombea mwenye umri mdogo kuliko wote jimboni humo ambaye amelelewa na CCM kuanzia Chipukizi hadi UVCCM na sasa anaelekea kuwania nafasi ya kuwatumikia ubunge mjini Moshi na kauli yao mbiu wananchi hao ni "Nuru Mpya ya Mabadiliko katika Umma "

No comments: