Familia ya Mang'ulo na ndugu Isaac Kibodya wanasikitika kutangaza kifo
cha bwana Abbas Khalfani Mang'ulo (68) ambaye ni baba mzazi wa Khajat
Swalha Kibodya, mke wa bwana Isaac Kibodya kilichotokea Bagamoyo,
Tanzania. Mazishi yamefanyika leo mchana huko Msata, Mkoa wa
Pwani. kwa hapa Marekani msiba upo nyumbani kwa bwana na bibi Kibodya
58 Vail Street, Springfield, Mass.
Dua imepangwa kufanyika Jumapili
Julai 19 Masjid Al Baqi 148 Fort Pleasant Avenue, Springfield, Mass
kuanzia saa 10 jioni mpaka saa mbili usiku. Kama ilivyo ada mnaweza
kutoa mkono wa pole kwa wafiwa kupitia simu namba # 413 219 1153
Wabillah Toufiq, Asalaam aleikum tujuike kuwafariji wafiwa.
No comments:
Post a Comment