ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 18, 2015

Naibu Waziri January Makamba amemtolea


Naibu Waziri January Makamba amemtolea
uvivu mshauri wa zamani wa Siasa wa Rais Jakaya Kikwete, Kingunge
Ngombale-Mwiru kwa kuupinga mchakato wa uteuzi wa mgombea wa Urais kwa
tiketi ya CCM na kusema anakivuruga chama.
Kingunge kumpigania mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani Edward
Lowassa, amekuwa akitoa matamko mbalimbali kuhusiana na mchakato huo
akisema haukutenda haki hasa baada ya kuenguliwa jina la Lowassa
ambapo baada ya mchujo wa majina likapatikana jina la mgombea mmoja,
Dk John Magufuli.

“Mzee Kingunge ni mtu mzima, ninamuheshimu sana, ni mkongwe katika
siasa, lakini anakivuruga chama… Ndani ya chama kuna wazee wenye
busara ambao waliangalia vitu vingi hadi kumteua mgombea kwani unaweza
kuwa mtendaji mzuri lakini ukawa na kasoro nyingi hivyo, unaweza
vilevile kuonekana ukashindwa kukivusha chama kwenye ushindi”—January
Makamba.

“Mimi ninamuheshimu sana Mzee Kingunge, lakini siwezi kukubaliana naye
anavyokandia mchakato. Mimi ninaamini ulikuwa sahihi, kila mtu
ameridhika na ndiyo maana kura zilipigwa”—January Makamba.

Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho, Mzee Yusuph Makamba alisema kwamba
watu wanaoendelea kulalamikia mchakato wa kumpata mgombea Urais kwa
tiketi ya CCM, wana masilahi binafsi na siyo kwa ajili ya kukiimarisha
chama hicho.


Mwanzoni mwa wiki, Katibu huyo wa zamani wa halmashauri kuu ya CCM
Mzee Kingunge alisema Kamati ya Usalama na Maadili iliteka majukumu ya
Kamati Kuu baada ya kuamua kuchuja majina ya makada waliojitokeza
kuwania urais hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo zilifanywa
kwa kuvunja kanuni na zililenga kumuengua Lowassa kuwania kuingia
Ikulu.

2 comments:

Anonymous said...

Well said, Mr. Makamba. Afterall, for decades, Mzee Ngombare-Mwiru has been a beneficiary of political corruption. Was he promised something from Lowasa? maybe. Let us bear in mind that, his age is a factor, medically speaking. Huku ughaibuni, angekuwa kwenye Assisted living, kwa sababu anahitaji muongozo katika maamuzi yake ya kila siku. I wonder, what advise alikuwa anampa LOwasa, it should be the other way round.

Anonymous said...

Huyu mzee anaongelea hitilafu zilizojitokeza kwenye uchekechuaji ambapo majina yaliyorudishwa yalikuwa machache na hakuna aliyeweza kusimama na kuelezea vigezo vilivyotumika kuchagua majina yenu matano. Kila mwana CCM anajua pendeleo la JK ilikuwa ni Membe na wewe January. Ni hasira za wapambe wa Lowassa ndizo zilizowaondoa wewe na mwenzako kwenye top five. Vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine leo hii. Ni bahati mbaya nyie badala ya kujibu hoja za mzee Kingunge, mnaongelea kuhusu changuo la Mheshimiwa Magufuli ambaye kwa bahati nzuri amepitishwa pasipo matarajio ya wachache wenye nguvu. Kweli hii ndiyo demokrasia tunayoiongelea na kuipigania?