
Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.

Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.

Mwandishi akiuliza swali kwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere ambaye leo alikutana na waandishi habari juu kuhama chama hicho na kurejea CCM katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam.

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini maelezo ya Mbunge wa Viti Maalum Chadema,Leticia Nyerere juu ya kuhama kwake katika chama hicho katika ukumbi wa idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.
MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mara ,Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam,Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.
3 comments:
HII NI YA MFA MAJI
Mimi naona ishakuwa fashion hiyo sasa kuhamahama vyama.
Huyu ni mbunge wa viti maalum. Anaweza kwenda popote anapotaka. Kwani alipachikwa tu. Isitoshe kaka yake alishatoka ccm na akaishia kurudi hukohuko ccm.
Post a Comment