ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 18, 2015

SALAMU ZA EID MUBARAK KUTOKA HOUSTON, TX



 Abou wa Houston. TX  mdau wa Vijimambo akiwa na mtoto wake Abou Jr  baada ya sala ya Eid. Abou anatoa salamu za Eid kwa waislam wote na Watanzania popote walipo.

 Abou akipata ukodak na Jr ndani ya msikiti huko Houston. TX
Ukodak pamoja na maustadh wenzake baada ya sala ya Eid

4 comments:

Anonymous said...

About Barnes,Eid Mubarak
Maas

Anonymous said...

Habari mdau
Samahani hii ni nje ya mada.
Mimi ni mbongo naishi Tanzania na ninaye mchumba mmarekani, tunataka tuoane na tukaishi kwao yaani USA.
Swali kwa wadau mnaoishi marekani.
Vp maisha ya huko nikiwa na mke mmarekani yanalipa na naweza nikafanya mambo mazuri nyumbani bongo?
Je miji gani inayolipa mishahara mizuri na salama?
Elimu yangu ya kidato cha sita, je kazi zipi ntakazo pata huko au lazima nichukue degree ndio maisha yatakuwa mazuri?
Naombeni wabongo mnaoishi USA mnijibu kabla sijafanya uamuzi wa kuja huko.
Tafadhalini bila kutumia lugha ya matusi

Anonymous said...

bila ya samahani lakini pia tupia swali lako katika jamiiforums.
mimi nitajaribu kukujibu kwa kadri ya uwezo wangu na kwa roho kujunfu na safi bila ya chenga.

nataka kukuliza kwanza maswali.na nataka uyafanyiye homework.

shemeji yetu ni mweupe au mweusi mwenzetu kwa ngozi?si tatizo na wala sitaki kukuingilia zaidi.ila it matters.kuna state na vitongoji vya mijii midogo midogo wanaubaguzi wa rangi bado.sikutishi ila nauliza tu nikutahadharishe.
Anaishi state ghani huku?anafanya kazi ghani huku?ana elimu ghani huku? ukifunguka zaidi ni rahisi watu kuchangia na kukujibu.tena kule jamiiforums ndo watakujifu kifasaha zaidi.

lazima uwe na malengo;jiulize unakuja huku kufanya nini?na usichukuliye kirahisi rahisi kwamba nataka kukaa miaka hii halafu nasepa home.watu walikuja na mipango hiyo hiyo na wanaserelea hadi hii leo.

usiwe na pupa na maisha,panga mikakati yako.umemshamsoma shemeji yetu ni mtu wa aina ghani je anaweza kuwasaidia huko kwenu.kumbuka mila na tamaduni zetu si sawa.huku watu hawana utamaduni wa kukaa na kusaidia ndugu zako kama hujitumi mwenyewe.

cha muhimu uwe na makaratasi/paper paper,ndo itakuwezesha kupiga boksi na kusoma na kurudi nyumbani unapojisikia.bila karatasi usisikiye utapata msoto hata kama utapiga boksi.

zidisha elimu yako,huku elimu ndo kila kitu asikuambiye mtu kitu si lazima kupata madegree lakini ukitaka unaweza kupata.The more you learn the more you earn.

miji mikubwa kama mfano L.A,Chicag NY,D.C, etc kuishi poa lakini kupata nyumba ni ghali ukitoka njee ya mijii mikubwa unaweza kuishi fresh na kujitanua tatizo uwe na gari.bila ya gari utapata taabu sana. mijii mikubwa hata kama huna gari,public transportation zipo. kibao.unaweza kupanda busi,ma subways(train)etc. change moto kwenye rent.

Maryland kuzuri kuishi;hata ohio,indiana,denver,cororado etc.
epuka vikundi vya marafiki wa mipasho pasho,huku hakuna vijiwe vya kukaa na kupiga story kama home;nyama choma unachoma mwenyewe na kama washikaji wako off ndo utawapata.

uwe mchapa kazi hakuna kulala lala na goi goi itakula kwako.maisha kuchapa kazi huku.na ukijisikia lonely jikazee si una mkee usichepuke ovyoo huku.otherwise utakuwa unalipa child support pesa zote zikamalizika na ukawa huna kitu cha kutuma home.

nakutakia kila la kheir usiogope wewe kidume cha mbegu karibu marekani.uafanikiwa tu ukiwa na malengo.kumbuka jichanganye na watu;usimdharau mtu hata kama una maisha mazuri msaidiye binadamu mwenzako.hujui nani atakuja kukusaidia wewe.

kazi na kusoma ukipaga makaratasi kama kichwani kipo fresh.kazi za kupiga boksi kwa sasa kwa elimu yako zipo wewe nguvu yako yakujituma,utashanga wapiga boksi wanajenga na kufanya ya maana huko nyumbani.ukitaka sana usomi unafuta degree mpaka phd.unaaza na vikozi vidogo vidogo hata IT,Kuwahudumia wazee,kazi ya nurse state zote ukiwa na ujuzi huu utachagua kazi yani wee mpaka basi.kazi za ulinzi madukani,mashuleni,maofisini.ni certificate tu huku unajiongezea zaidi elimu.maisha mapambano usijali utafanikiwa tu mkuu.karibu sana marekani.

feel free ukiwa na swali la ziada.tupo pamoja mkuu.mungu awe nawe daima utafanikiwa tu karibu marekani.

Anonymous said...

aaah mkuu wewe kweli umempata wife wa kimarekani au unataka kuzamia meli,seaman baharia.ulivyo uliza nimekusoma hivyo.wacha longo longo zamia tu meli ibuka njoo upige boksi na mtaji wako kiuno utawapata totoz zitakupa karatasi.jikaze buti be a soldier ukiwa lege lege huwezi zamia meli.

na msela bi toz upo wapi TZ?