Advertisements

Tuesday, July 28, 2015

TABATA SHULE YA MSINGI YANUFAIKA NA MSAADA WA MADAWATI 100 TOKA BENKI YA KCB TANZANIA

 .Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta akikabidhiwa msaada wa madawati 100 na Meneja Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City, Benjamin Mgonja(kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo.Benki hiyo imetoa msaada wa matawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB Tanzania wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Tabata.Wakati wa hafla ya  kukabidhiwa msaada wa madawati 100 na Benki hiyo jana.
 Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi Tabata wakibeba madawati kuyapeleka madarasani baada ya kukabidhiwa msaada  wa madawati 100 na benki ya KCB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mradi wa madawati 1000 kwa shule za msingi 10 za msingi jijini Dar es Salaam.

  Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Tabata ya jijini Dar es Salaam,Tumaini Kabuta(kushoto)akiteta jambo na Meneja Biashara wa Benki ya KCB Tanzania, Tawi la Mlimani City Jijini Dar es Salaam, Benjamin Mgonja wakati wa hafla fupi ya makabidhino ya  msaada wa madawati 100  kwa shule hiyo.Benki hiyo inaendelea na kampeni yake ya kutoa  msaada wa madawati 1000 kwa shule kumi za jijini Dar es Salaam.
.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Tabata jijini Dar es Salaam, wakionyesha mshikamano na furaha baada ya kupokea msaada wa madawati 100 kutoka Benki ya KCB Tanzania wakati wa hafla fupi iliyofanyika shuleni hapo jana.

No comments: