
Mkurugezi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary (mwenye kanzu) akimwonesha Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Mha. Happiness Mgalula sindano iliyochambuliwa na mashine ya kuchambua uchafu kwenye alizeti inayoletwa kiwandani hapo. Anayetazama ni Mha. Omari Athumani, Mchambuzi Sera Mkuu, Tume ya Mipango

Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akiwaonesha wajumbe wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango machine ya kukamua mafuta ya alizeti (haionekani pichani)

Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha kupakia mafuta kwenye madumu wakiendelea kupakia mafuta ya ujazo wa lita tano kiwandani hapo

Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta cha Singida Fresh Oil Mills Khalid Omary akionesha dumu la mafuta yanayozalishwa na kiwanda chake tofauti na yale ambayo ni feki ambapo watu wasio waaminifu wanatumia nembo ya kiwanda hicho

Baadhi ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wakisubiri huduma ya kukamua mafuta kiwandani hapo. Takribani asilimia 80 ya wakulima wanaoleta alizeti kiwandani hapo wanataka kukamua mafuta ambapo kiwanda kinawalipisha gharama ya kukamua lakini wao wanaondoka na mafuta yao. Jumla ya wakulima 500 wanaleta alizeti kiwandani hapo.
1 comment:
kwenye picha ya kupakia mafuta! mbona kama ni watoto wanaofanya hiyo kazi? au macho yangu? kama ni watoto please waende shule na kiwanda kiwasomeshe!!!!!
Post a Comment