ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 10, 2015

URAIS CCM: TANO NA TATU BORA KUPATIKANA LEO


Baadhi ya waandishi wa habari waliopo mjini Dodoma, wakiirusha taarifa hiyo baada ya kuipata, leo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ametoa ratiba ya Vikao kwa siku ya leo tarehe 10/7/2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nape amesema, kuanzia Saa 4 hadi saa 7 mchana, kitafanyika kikao cha Usalama na Maadili chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.

Amesema kuanzia Saa 8 hadi saa12 Jioni ni Kikao cha Kamati Kuu kitakachopitisha majina matano ya wagombea walioomba ridhaa ya CCM kuwania Urais.

Nape amesema na Saa 2 usiku baada ya waliofunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kufuturu, kitafanyika
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), kwa ajili ya kupitisha majina matatu ili Mkutano Mkuu utakaoanza kesho asubuhi upokee majina hayo na kumchagua mmoja wapo atakayepeperusha bendera ya Chama.

SABABU YA KUCHELEWA VIKAO NA HASA KUTOFANYIKA JANA:
Nape amesema ratiba ya vikao ambayo ilikuwa imetolewa awali haikufuatwa kwa sababu ya Shughuli zilizojitikeza za Mhe Rais za Kichama na Serikali ambazo amekuwa akizifanya tangu alipowasili Dodoma juzi.

Amesema, sababu nyingine ni kuwepo kwa Vikao vya mashauriano, ili kuhakikisha kuwa vikao vya mchujo vinaisha kwa salama na hatimae Mgombea wa CCM apatikane kwa Amani.

1 comment:

Anonymous said...

Bado CCM hawana mgombea safi hatabwakikaa vikao kumi wote ni walewale. Kwani wakishaingia mambo yanabadilika na kujijali wenyewe na waliowaweka madarakani. Rudisheni fedha ya Escrow na ya mabehewa feki. Fedha iliyotafunwa kweupe trl 1.15 iko wapi ??