Wednesday, July 8, 2015

UVCCM NYAMAGANA WAMUWEKA LOWASSA NJIA PANDA.

Hussein. A. Kimu Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza.
Wanahabari

YAH.TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO.

Ndugu wanahabari na watanzania wote. Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote.

Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi, Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea,kuonya,kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya Wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa.

Cha kusikitisha Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu
anae jiita mtemi Sylvester Yared. ambae ndio mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa mwanza. Binafsi nilishitushwa sana

Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu 
1.Jumuiya ya wanawake(UWT) 
2.Jumuiya ya wazazi 
3.Jumuiya ya vijana (UVCCM) Ndani ya cham cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement. Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa.

Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga,wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowasa. 

Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke.

Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu.

Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania.

Imeandaliwa na
 Hussein. A. Kimu 
Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza.

4 comments:

Unknown said...

Kwanza kabisa huwezi kuwa mwana chama,ndani ya chama ukatoa matamshi ya namna hii. Kwa vyovyote vile wahusika watakula sambamba na wewe kusudi useme ukweli wa haya unayoyasema. Kilicho mkuta Mrema kila mtanzania anakikumbuka. Hata yeye mwenyewe anajutia .maneno yake. Acheni uchochezi usio kuwa na maana. Kama unataka nenda Dodoma ukawaeleze wajumbe wa mkutano mkuu. Shukuru mungu Tanzania hatufuati sheria.

Anonymous said...

Byamungu una mgongano wa maslahi katika hili jambo. Toa hoja zako baada ya July 12, 2015! Hata hivyo, pole sana kwa sababu ENL hatapenya kwenye mchujo hata ule wa kwanza tu. Usinywe sumu lakini, kwa sababu nduguzo bado tunakuhitaji waitu!

Isaiah said...

CCM imejijengea utaratibu wa kumpata kiongozi wa nchi kupitia chama chake kwa muda mrefu sana. Yeyote anaye taka kugombea oungozi wa nchi kupitia chama hicho analazimika kutii na kufuata utaratibu huo. Kama mtu atatokea kuomba ateuliwe na chama hicho kwakutumia njia zake mwenyewe nje ya zile zilizowekwa na chama, atakuwa anawafanyia fujo wanachama wenzake wanao taka kufuata utaratibu huo.

Ikiwa atakuwepo mgombea ambaye anaona CCM inamapungufu katika utaratibu wake, basi anaweza kwenda kugombea nafasi hiyo kwa kutumia chama kingine bila kusababisha vurugu na fujo. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amefanya kazi nzuri sana akiwa kamanda wa majeshi ya ulinzi ya mkoa wake. Ningekuwa ni mimi ningefanya hivyo hivyo alivyo mkuu huyo wa mkoa. Na mimi naungana na kiongozi wa u,oja wa Vijana wa CCM Wilaya Mwanza, Nyamagana, Kuwa uongozi unaoweza kupatikana kwa njia aliyoieleza haufai katika jamii ya watanzania.