ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 20, 2015

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV NA WASHIRIKA WAO WAWASILI SALAMA TANZANIA NA KUTOA MSAADA WA MADAWA HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR LEO

Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Idd Sandaly mwenye fulana nyekundu wakifanya maongezi na Mkuu wa kitengo cha Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimaifa Bi. Rosemery Jairo siku Viongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV na washirika wao wakiwemo manesi na madaktari wa kujitolea walipowasili Tanzania kwa ajili ya kutoa huduma za kitabibu na madawa bure katika hospitali mbalimbali Tanzania.
 Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Idd Sandaly akiwa katika picha ya pamoja na mama Mukami walipokutana katika hospitali ya Mwananyamala leo Jumamtatu July 20, 2015 Uongozi wa DMV na washirika wake walipokwenda kutoa huduma za kitibabu na msaada wa madawa ya bure.
Kushoto ni Joha Nyang'anyi akisaidia kupaki madawa siku ya Alhamisi July 16, 2015 Greenbelt, Maryland kabla ya kusafirishwa kuelekea Tanzania na Jumuiya ya Watanzania DMV wakiwemo washirika wake wakujitolea. Kulia ni Dr. Sylivia Dassi ambaye ni mmoja wa madaktari waliojitolea kwenda Tanzania kutoa huduma za kitabibu katka hospitali mbalimbali Tanzania.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV na washirika wake wakiwa kwenye basi kuelekea hospitali ya Mwanannyamala mapema leo Jumatatu July 20, 2015.

Kundi la vijana la DMV lililojitolea kushiriki katika zoezi hili likipata picha ya pamoja wakiwa hospitali ya Mwananyamala mapema leo Jumatatu July 20, 2015. Kati ni Asha Nyang'anyi ambaye nae yupo kwenye msafara huo.

 

1 comment:

Anonymous said...

Bravo! So Proud of the Work you all are doing for Tanzania !
Young diaspora youth are watching and learning from you !