ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 23, 2015

WANAFUNZI DARASA LA SABA SHULE YA ADOLPH KOPING BUKOBA WATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI KAGERA.

Wanafunzi wa Darasa la Saba (Adolph Kolping English Medium Primary School) wametembelea kiwanda cha Kagera Sugar kilichopo Bukoba na kujionea utengenezaji wa Sukari ikiwa ni sehemu ya mafunzo yao.
Kiwanda cha Sukari cha Kagera tayari kilishaanza kuzalisha ziada ya sukari inayohitajika katika soko la sukari Nchini hali inayopelekea kuweza kupunguza tatizo la upatikanaji wa sukari Tanzania na Nchi za jirani zinazotumia sukari kutoka kiwandani hapo.
Kiwanda hicho cha Sukari cha Kagera kiko katika sehemu Kaskazini Magharibi ya Tanzania (karibu na mpaka wa Tanzania na Uganda) kilibinafsishwa na Serikali kwa sekta binafsi mwaka 2001. Malengo ya ubinafsishaji yalikuwa kuboresha upanuzi wa masoko ya ndani na kikanda, uwekezaji wa kisasa, upanuzi na ukarabati na majengo ili kuhakikisha shughuli za kiundeshaji zinaboreshwa.

Daraja la Mto Kagera
Mto wa Kagera ni kati ya mito inayounda mto wa Nile pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.
Inaanza Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo na Ruvuvu ikiendela 400 km hadi kuingia ziwa la Victoria Nyanza.
Mto wa Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale inapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho wa njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza kama 40 km kaskazini za Bukoba. Jina la Mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.
Wanafunzi wa hao wa darasa la saba walipata nafasi wakapita Darajan hapo na kuweza kujionea taswira kamili ya Daraja hilo. Wengi wa Wanafunzi hao walikuwa hawajawahi kupita hapo. Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Picha ya pamoja ikapigwa
Wengi wakafurahia!
Wanafunzi wakitokelezea pamoja na Mwalimu wao wakati wa safari hiyo
Wakiingia Eneo la lango kuu la Kiwanda hicho cha Kagera Sugar. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo
Rev. Sr. Merceline Masha. Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Wanafunzi hao waliongozwa na Walimu wao katika Ziara hiyo
Mfanyakazi wa Kiwanda cha Kagera Suagar Bw. Moses Mwanga akitoa maelezo kwa Wanafunzi hao juu ya Kiwanda hicho akianzia Historia fupi ya kiwanda tangu kilipoanzishwa na Baba wa Taifa mwaka 1982 hadi kilipobinafsishwa mwaka 2011 na mpaka sasa.Kisomo kikiendelea...Bw. Moses Mwanga akitoa ufafanuzi juu ya aina ya Miwa inayolimwa katika Mashamba yao.
Miwa ikitolewa Shambani upimwa na kumwagwa eneo hili na kisha uongozwa kwa mashine ndani ya kiwanda.
Wanafunzi wakijionea hatua ya pili baada ya kukatwa katwa miwa bila kukamliwa na kisha kwenda hatua nyingine.
Wafunzi wakiendelea kujionea shunghuli mbalimbali ndani ya kiwanda hicho.
Sehemu ya Jiko
Wanafunzi wakipata kuonja sukari hiyo inayopatika hapo kiwandani baada ya kujionea tangu Miwa inatoka shambani mpaka uundwaji wake!
Bw. Moses Mwanga akiwa ndani ya Maabara ya Kiwanda hicho akitoa maelezo kwa Wanafunzi, Habari na Picha na Faustine Ruta, Bukoba
Mkuu wa Shule Rev. Sr. Merceline Masha akiwaongoza Wanafunzi
Maji kutoka Mto Kagera ufikia eneo hii na kuchujwa kwa Mitambo na kuwa salama na tayari kwa kutumia kwa shughuli mbalimbali kiwandani hapo.
Kutenganisha Tope na maji
Mwisho waliweza kukutana na kuuliza maswali ya hapa na pale na kujibiwa mtaalam Bw. Moses Mwanga.

No comments: