ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 13, 2015

WATANZANIA NA WANA CCM WOTE WA TAWI LA NEW YORK.

Ni takribani siku 29 zimepita
tangu marehemu Alfred Magege alipo aga dunia mnano 6/13/15 na kuzikwa
6/28/15. Familia ya marehemu bado haijasahau na haitasahau moyo wa
pekee uliojaa upendo, faraja, ukarimu, umoja, mshikamano, undugu na
urafiki wa kweli wakati wa kipindi hicho kigumu cha msiba.
Kushiriki kwenu kumeipa familia imani, sababu, na nguvu
nyingine ya kuendelea kukabili maisha pasipo hofu tukitambua familia
kubwa iliyotuzunguka kipindi hicho na Mwenyezi Mungu anayetunza siku
kwa siku tukiwa hapa duniani. Tunatambua kuwa haikuwa rahisi hata
kwenu, Ila kwa moyo mlijitoa kuwa na familia tangu mlipo pata habari
marehemu yuko hospitalini na hata alipotuacha. Shukrani zetu hazitoshi
kushukuru kwa yote mliyotutendea. Wakati huo tulihitaji watu wa
kuomboleza nao na mlikuwepo kuomboleza pamoja na sisi. Mmetumia mda
wenu kuja hospitalini na hata nyumbani baada ya
msiba, mlijitoa kupika usiku na mchana siku zote tangu msiba
ulipotokea mpaka mwisho. Mmetoa michango ya kila hali zikiwemo pesa,
ambazo zimesaidia sana kukamilisha shughuri hiyo nzito ya mazishi.

TUNAOMBA MPOKEE SHUKRANI HII YA PEKEE KUTOKA KWETU. ZAIDI TUNAWAOMBEA
KWA MUNGU WA MBINGUNI BARAKA NA MAFANIKIO KATIKA SHUGHURI ZENU ZOTE
MFANYAZO. MUNGU AWAZIDISHIE MARADUFU PALE MLIPOTOA. 

Geoffrey Ngullu.

No comments: