ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, July 23, 2015

WIZARA YA MAMBO YA NJE YAMUAGA RASMI BALOZI WA UBELGIJI ALIYEMALIZA MUDA WA KAZI NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akitoa hotuba wakati wa kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Mhe. Adam Koeler huku Balozi huyo (wa kwanza kulia waliketi) na wageni waalikwa wakimsikiliza. Hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai, 2015. Katika hotuba yake Balozi Kasyanju alimsifu Balozi Koeler kwa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Ubelgiji. 
Balozi Koeler pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine wakimskiliza Balozi Kasyanju wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi Koeler. 
Balozi Koeler nae akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga. Katika hotuba yake Balozi huyo aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kusifu ukarimu wa Watanzania. 
Balozi Kasyanju kwa pamoja na Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Congo (DRC), Mhe. Juma Halfan Mpango na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodrigues wakimsikiliza Balozi Koeler (hayupo pichani) akihutubia. 
Balozi Sokoine nae akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Koeler 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bunndala (katikati) akiwa na wageni waalikwa wengine wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (katikati) akiwa na Balozi wa Ujerumani hapa nchini, Mhe. Egon Kochanke (kushoto) pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Felister Rugambwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji. 
Balozi wa Ireland hapa nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan (kulia) akiwa na Bw. Rodrigues (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Maulidah Hassan wakati wa hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji 
Wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo 
Bi. Kasiga ambaye alikuwa msheheshaji (MC) katika hafla hiyo akiwakaribisha Mabalozi na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo 
Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju (kushoto) na Balozi Koeler (kulia) pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza Bi. Kasiga ambaye haonekani pichani 
Juu na Chini ni Maafisa Mambo ya Nje wakifuatilia matukio kwenye hafla ya kumuaga Balozi wa Ubelgiji. 
Balozi Koeler akiteta jambo na Balozi Sokoine 
Balozi Kasyanju, Balozi Koeler na wageni waalikwa wakitakiana afya njema 
Balozi Koeler akifurahia zawadi ya picha ya kuchora ya Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro aliyokabidhiwa na Kaimu Katibu Mkuu, Balozi Kasyanju huku akitamka kuwa "nitarudi Tanzania kuja kupanda Mlima Kilimanjaro". 
Balozi Koeler akimshukuru Balozi Kasyanju kwa zawadi hiyo nzuri 
Picha ya Pamoja.

No comments: