ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 21, 2015

Wizara yawapokea Madaktari kutoka Marekani

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akiwakaribisha nchini Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka  Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania DMV.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bw. Iddi Sandaly (watatu toka kulia)ambaye amefuatana na Madaktari hao kutoka Marekani akielezea jambo mara baada ya kuwasili nchini. 
Bibi Jairo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu dhumuni la ziara ya madaktari hao hapa nchini. 
Mmoja wa Madaktari kutoka Marekani akizungumza na Waandishi kuhusu ziara yao hapa nchini 
Bw. Idd Sandaly akifafanua jambo kwa waandishi kuhusu ziara ya madaktari hao kutoka Marekani.

No comments: