ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 28, 2015

ABBAS MAZIKU: MFANYABIASHARA ANAYETAMANI KUFUATA NYAYO ZA BILIONEA MO DEWJI

04.jpgk
Mfanyabiashara wa Kimataifa Abbas Maziku akiwa katika picha ya pamoja na Mfanyabiashara ambaye pia ni Bilionea kijana Barani Afrika, Mtendaji Mkuu wa kampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji, 'MO' amabaye anafuata nyayo zake katika kufikia malengo yake kibiashara.

Na Mwandishi Wetu
BIASHARA ya kusafirisha mazao ni miongoni mwa biashara zenye ushindani mkubwa kutokana na kutawaliwa na matajiri wenye asili ya Kiasia.
Kutokana na sababu hiyo imewafanya waafrika wengi kuwa na uthubutu katika biashara kwa kuhofia huenda wasifanikiwe na kujitanua kibiashara.
Mbali na ugumu huo lakini pia waafrika wengi hasa watanzania wamejikuta wakiishia kuwa wafanyabiashara ya kawaida na kupoteza fursa za kimataifa .
Kupoteza fursa muhimu za kimataifa kumefanya wakose fursa ambazo zingeweza kuwafanya wawe na mawazo mengine ya kuchangamkia fursa za kibiashara na kufikiri nje ya boksi.
Makala haya ndani ya mtandao huu yanaangazia mahojiano na mfanyabiashara wa kwanza wa kitanzania kufanya biashara ya kusafirisha Korosho kwenda nchini Vietnam aitwaye Abbas Maziku ambapo alielezea alipoanzia, vikwazo, mafanikio na matarajio yake kibiashara.

Alipoanzia

Maziku anasema alianza biashara ya kusafirisha mazao mnamo mwaka 2013 baada ya kuvutiwa na mjomba yake ambaye alikuwa na mashamba yaliyokuwa na mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku alianza nayo na anaendelea nayo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Choroko, Mtama, Alizeti, Mashudu yapamba na pamoja na Pilipili Manga.

Anayapata wapi mazao?

Anasema mazao huyakusanya kutoka kwa wafanyabaishara wadogo wadogo ambao hukusanya mazao kwa wakulima pamoja na minada inayofanywa na vyama vya ushirika katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa kila wiki.

Anayasafirisha kwa njia gani?

Akizungumzia jinsi anavyosafirisha mazao hayo, Maziku anasema hutumia usafiri wa barabara kuyatoa mikoani hadi kuyafikisha kwenye maghala ambayo hutumia kuyahifadhi kabla ya kufungasha.
"Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa nayafungasha kwa kutumia vibarua na katika vifungashio vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina la kampuni yangu na baada ya hapo sampuli hupelekwa katika maabara za kupima kupima ubora wa mazao kimataifa iitwayo SGS na ndipo hufuatiwa na hatua ya mwisho ya usafirishaji ambayo huwa natumia Meli za mashirika mbalimbali ikiwemo IPTL, MAERSK na nyinginezo kwa ajili ya kwenda nchini Vietnam", anasema Maziku.
Anabainisha baada ya hatua zote hizo hufuata taratibu zinazotakiwa ikiwemo watu wa Mamlaka ya mapato T.R.A, wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo na Ufugaji, Wanasheria pamoja na maofisa wa usalama wa Taifa ambao uhakikisha hatua zote halali zimefutwa.
Maziku anaweka bayana kwamba kwa biashara za kimataifa taasisi kama Shirika la viwango TBS na mamlaka ya Chakula na Dawa huwa hawahusiki bali wahusika wakuu ni SGS.

Anajiendeshaje Kibiashara?

Maziku anajinasibu kuwa biashara ya mazao kupeleka nje ya nchi ni biashara yenye ushindani mkubwa hivyo anakumbuka alianza na mtaji wa sh 2,000,000 na sasa anazungumzia mtaji wa sh mil 200.
“Si rahisi kufika nilipofikia kwa sababu biashara hii ina ushindani mkubwa, ninashindana na matajiri wakubwa wenye uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo ingawa nimepiga hatua lakini bado ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na zaidi”, anasisitiza kwa hisia kali.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara ya mamilioni ya pesa baada ya ubora wa mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa hivyo ilimpa wakati mgumu ambao aliyumba kibiashara kutokana na mtaji wake kukata hivyo ili mlazimu kuingia benki na kukopa pesa ambazo hadi sasa bado analipa deni hilo.
“Nilipata hasara kubwa sana ambayo hadi leo hii bado ninalipa hilo deni nililokopa benki ingawa pia fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vya mapato ya biashara zingine ninazozifanya zinaendelea kuifanya biashara hii ya mazao kwenda nje ya nchi iendelee kuwepo” anasema Mfanyabiashara huyo wa kimataifa.
 

No comments: