Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Mh. Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha wamejiuzulu nafasi zao zote na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Katibu mwenezi amemtahadharisha katibu mkuu wa CCM, ache kuwaita Watanzania makapi.
ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAARIFA ZAIDI
3 comments:
Tanzania hatuhitaji siasa za kimajimbo au kabila la watu fulani ili tukisapoti chama fulani hayo ni mambo ya kipuuzi kwa nchi yetu. Mbona sisikii morogoro au shinyanga au songea kwamba watu wamehama kwa makundi kutoka CCM kwenda chadema au hiyo chadema si kwa ajili ya watanzania wote. Matokeo yote ya wana CCM kukihama chama yatokee Arusha au Kilimanjaro na wote wanahamia chadema sio CUF au ACT wananchi au L N D? Kulikoni jamani.
Hayo ni mawazo yako wewe anon hapo juu. Tukiangalia sehemu za SINGIDA, MOROGORO, LINDI, MTWARA, TABORA, DODOMA, IRINGA, PWANI,RUKWA,RUVUMA N.K mbona zina CCM toka Enzi na Enzi? Ina maana ni ukabila unaoletwa na CCM...siyo??? Uelewe kuna kitu kinaitwa stronghold, hizo sehemu unazozingumzia watu wana imani na sera walizomwagiwa na hivyo vyama,siku zote chama kinakuwa sehemu zinazoaminiwa na wananchi na pia inategemeana na Elimu na Uelewa wa wananchi wa sehemu husika. CCM haina hatimiliki ya nchi hii....pia uelewe pia Charity begin at home.....usitegemee CCM itashindwa Lindi au TABORA (Ndiyo maana umesikia Lipumba amerudi alikotoka ingawa bila kufahamisha umma anakokwenda)
Wewe acha spade iitwe spade; no sugarcoating! Mtu anakuwa mwanachama wa kweli wa chama fulani kwa kuamini sera na miongozo ya chama hicho, sio kwa sababu ya mwanachama mwingine fulani ndani ya chama husika. Kama sio ukabila na ukanda, hao wamasai na wachaga wanaohama CCM kwenda CDM wangefanya hivyo kabla ya Lowasa kukatwa au wangehamia ACT, NLD, UDP, DP, nakadhalika, ambako mgombea wao wa kikabila/kikanda hayuko.
Kwa kifupi, siasa za ukabila na ukanda hazitawafikisha kokote nchi hii, kwa sababu waasisi wa nchi hii hawakuijenga kwa misingi hiyo. Subirini kibano cha wana wa Tanzania ya Nyerere na Karume! Mnadhani hii ni karne ya umangi na ulaigwani. Tayari mnajua mlikoishia na ushabiki wenu wa Mrema enzi hizo. Wembe wa wana wa Tanzania ya Nyerere na Karume ni uleule!
Post a Comment