Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akimpongeza Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya kwa ofisi hiyo kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti , 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakifurahia kombe la kuwa mshindi wa kwanza kwa Wizara za Huduma za Jamii zilizoshiriki maonesho ya Nane Nane Kitaifa mkoani Lindi, Tarehe 8 Agosti , 2015, walioshika kombe hilo katikati ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya, kulia kwake ni Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe.
Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi akipata maelezo ya bidhaa zinazotengezwa na vikundi vya wajasiriamali kutoka Zanzibar waliowezeshwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Miundo Mbinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF) na kushoto kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maadhimisho ya Kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu, Flora Mazilengwe, walipotembelea banda hilo Tarehe 8 Agosti , 2015.
No comments:
Post a Comment