Advertisements

Sunday, August 30, 2015

Helikopta ya Nyarandu Anogesha Kampeni za Mgombea Mwenza CCM

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la  Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba. Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la
Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua. Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini ikitua.Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa kampeni na kuacha kushangaa helkopta.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua na helkopta. Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya kutua na helkopta.Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri. Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa inamsubiri.
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi. Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi.Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCM Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCMMjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni Iramba Magharibi.Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku. Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi. Mziku.Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba. Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea kunadiwa jimboni Iramba.

Na Joachim Mushi, Singida MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea ya kuinadi ilani ya CCM. Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa ni muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za wanaCCM na wananchi katika mkutano huo. Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge alitumia helkopta hiyo kwenye mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya Jimbo la Iramba Magharibi. Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura CCM kwani ndani ya ilani yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa maendeleo ya mkoa huo. Alisema endapo watachanguliwa watajenga kiwanda kikubwa cha kusafishia mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza thamani ya mazao kwa wakulima wa eneo hilo. Aliongeza kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia kitatoa nafasi za ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600 watapata ajira ndani ya kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya awamu ya nne kujenga shule za Sekondari za kata za kutosha na maabara ilani mpya ya CCM imepanga kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo ili ziweze kutumika kwa ufasaha. Bi. Suluhu alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya rufaa ambayo itakuwa ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani, pamoja na ujenzi wa barabara ya Ndago. Aidha akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi kufanya jitihada za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili kusongeza huduma kubwa za afya kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme vijiji ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) awamu ya pili. Aliongeza kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio la ukame aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo hayo. "...Serikali imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba ya kutosha, hivyo niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa njaa. Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza jimboni hapo alisema ilani ya CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji katika Vijiji vya Mgundu, Kinampanda, Makunda pamoja na vijiji vingine vinavyokabiliwa na kero ya maji. Alisema baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata kufanikiwa serikali itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa mabweni ili kuwanusuru watoto wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni pamoja huku wasichana wakikabiliwa na changamoto za kubebeshwa mimba na kukatishwa masomo yao. Mwingulu aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja za msingi na vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha. Bi. Suluhu anaendelea na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma akiinadi ilani ya CCM.

9 comments:

Anonymous said...

Sasa mbona kuna DOUBLE STANDARDS TANZANIA CIVIL AVIATION?

Anonymous said...

Unatua na helkopta wakati kuna mama anatembea na ndoo ya maji kichwani, serikali gani hii ilibidi hudumaa muhimu kama maji yatoke kwenye mabombaa yaliyo ndani kwake. Na kama hana mabombaa ya maji ndani haustaili kuwa na hiyo helkopta naamini karne hii ya 21 kila Mtanzania ilibidi apate mahitaji muhimu pale alipo na sio kwenda kuteka maji wakati Nyalandu anaruka na helkopta mke wa Nyarandu kwake anaendaga kuteka maji na kuyabeba kichwani mpaka nyumbani?

Anonymous said...

Si Helikopta zilikatazwa?? sasa mbona CCM wanatumia?

Anonymous said...

Meno ya Tembo yanakamatwa uswis angetakiwa kujiuzuru uwaziri mara moja. Bado unatumia Helicopter kuomba ubunge hela za kufanya kampeni Kama hiyo anapata wapi Kama ni muajiriwa wa serikali hata mgombea urais anasafiri kwa magari. Huu ni ujinga wa nyarandu na sisiemu hawafiki waTZ wanyonge wanateseka kama huyo mama amebeba ndoo ya maji. Ndiyo maana UKAWA unakuja kuwakomboa wananchi mwaka huu

Anonymous said...

Kama unaushahidi mpeleke mahakamani. Huna ushahidi nyamaza..

Anonymous said...

Aliomba kibali.Over...

Anonymous said...

Toa mfano wa nchi ya inayoendelea ambayo kila raia anabomba la maji ndani ya nyumba yake.Hata nchi za second World ( Brazil,India) hilo halipo..

Anonymous said...

Nani kasema Helicopter zimekatazwa.Unapaswa kufuata utaratibu na upewe kibali na mamlaka husika.Acha upotoshaji..

Anonymous said...

Helikopta za kulinda tembo zinatumiwa kwenye shughuli za siasa ambulance za kubebea wagonjwa ndo gari la kupeleka madaktari nyumbani. Bongo