
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda jana. Picha na Said Khamis
Dar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini jana jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita.
Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.
Akihojiwa na Azam Tv kwa simu akiwa Kigali, siku tatu baada ya kuondoka nchini, Profesa Lipumba alisema alikuwa nchini humo akifanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa katika sekta hiyo.
Alipoulizwa jana, Profesa Lipumba alisema akiwa huko alikuwa na mazungumzo na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda (RDB), wadau wa masuala ya rushwa, waziri wa fedha wa nchi hiyo na makamu mwenyekiti wa Bodi ya Utawala.
“Wenzetu wamepiga hatua kubwa katika kukuza uchumi ndani ya kipindi kifupi, hivyo safari yangu ilikuwa ya kujifunza mbinu walizotumia kufikia malengo yao,” alisema.
Akizungumzia hatima yake kisiasa, licha ya kusema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, alisema hatashiriki kufanya kampeni kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa kuwa umoja huo umemsimamisha mwanachana wa CCM, Edward Lowassa.
“Kisiasa hatima yangu ni kama ya Mtanzania mwingine yeyote, Ukawa tuna mgombea kutoka CCM, amehama juzi tu, pia mle ndani ya Bunge la Katiba hakuunga mkongo Rasimu ya Katiba na ndiyo maana nikasema dhamira yangu inanisuta,” alisema Profesa Lipumba.
Alisema wanachama wa CUF hawana sababu ya kuona kama amewaacha kwa kuwa bado yupo nchini.
Awali, akitangaza kujiuzulu, nguli huyo wa uchumi, alisema alifikia uamuzi huo kutokana na Ukawa kumkaribisha Lowassa kugombea urais kupitia umoja huo, hivyo dhamira yake inamsuta.
7 comments:
Huyu alitajwa na Lowassa kuwa yupo kwenye payroll ya CCM ndo maana alikimbia. Lowassa peke yake angesupport katiba ingepita?
huyu kesha kula pesa ya ccm sasa anakuja kufanya kazi ya watu,hakuna uprofessa hapa huyu anachumia tumbo siku zote sasa tumefahamu karibu ccm wanakuhitaji wakati huu kuliko UKAWA tafadhali kawafanyie kazi zao kwa ufanisi zaidi lakini sisi ukawa basi muhimu nchi sio maneno mengi,bora ukajiunge na ccm iwe tume badilishana sisi tumechukua Lowassa na wao tuna wapa Lipumba kwaheri mzee safari njema.
Uzuri wananchi wana ufahamu mkubwa, prof lipumba pumzika baba,watu wana hasira wasije wakakupopoa na mawe bure.
Kwanza huyu alitakiwa akamatwe lakini nkwa kuwa alitumwa na wenyewe basi akae alivyo na hahitajiki kwa upande wowote. Lipumba unaonekana kabisa huoendi maendeleo ya waTanzania wengi wanaotaabika na ulipokuwaa unadai kuweza kuwatumikia waTanzania ulikuwa unadanganya toto hufai kabisa na hatutashangaa kukuona kwenye kampeni za CCM. Huu ni ujuni ndani ya nchi yako msomi wa aina gani na unaaminika wapi sasa. Anzisha chama yako.
kwenye fisadi EL mtamuosha na madodoki, maana mlisema ni mchafu,ananuka,papa fisadi. vipi anafaa. kweli mfaa maji haishi..... malizia nyie washabiki wa chadema. mtaspin sana mwisho wenu oktoba na mtalia sana. ccm ina utaratibu wa kusimamisha mgombea safi anayepigiwa kura na wajumbe sio huyo papa fisadi aliteuliwa na wafanyabiashara wenu wa Kilimanjaro. soma alama wewe
Anachosema huyu jamaa kinalingana na serikali ya CCM huko nyuma kumuita kaburu mtu mbaya sana. Leo hii kaburu ndiye mwekezaji kwenye madini, gesi nk. Ari yetu ni moja " Toa CCM ikulu ingia Ukawa"
Anonymous wa11:02am,inaonekana wewe ni mtoto wa balozi wa mtaa wa nyumba kumi kumi CCM,eti wafanya biashara wa Kilimanjaro?wewe endelea kuota ivyo ivyo na propaganda za ukabila,na shughuli ya mbeya leo ni wachaga si ndio?
Post a Comment