Hamfrey Polepole na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa wamekabana kwa hoja kali kuhusu uamuzi wa Chadema na Ukawa kwa ujumla kumpokea Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea Urais.
Polepole na Msigwa walikutana jana katika kipindi cha ‘Mada Moto’ kinachorushwa na kituo cha runinga cha Chanel Ten kujadili mada iliyotajwa kama ‘Lowassa Ndani ya CCM’.
Polepole alionesha msimamo wake wa kumkataa Edward Lowassa kuwa sio kiongozi sahihi aliyepaswa kuungana na Ukawa katika safari yao ya kutaka kuongoza dola na kupata katiba mpya ya wananchi kwa kuwa ana tuhuma nzito zilizompa madoa.
Aliongeza kuwa dhana ya upinzani na mwenendo wa Ukawa ulipotea pale walipomkaribisha Lowassa huku wakisahau kuwa ni miaka michache iliyopita walizunguka nchi nzima kuwaaminisha watanzania kuwa ni fisadina kwamba wana ushahidi wa kutosha.
Polepole ambaye alikuwa mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iyoongozwa na Jaji Warioba, alisema kuwa Ukawa iliundwa kwa madhumuni ya kutetea Katiba ya Wananchi na sio kwa lengo la kisiasa kama ilivyo sasa.
Alisema kuwa Edward Lowassa hana msimamo thabiti kwenye maamuzi yake kuhusu Katiba anayoitaka kwa kuwa aliwahi kumhoji awali akasema anahitaji muundo wa serikali tatu lakini baadae alimfuata na kumueleza kuwa amebadili anataka muundo wa serikali mbili.
“Lowassa niliongea naye wakati huo nakusanya maoni kuhusu katiba mpya, mara ya kwanza alisema anataka serikali tatu na akaandika kwenye kumbukumbu maalum za bunge. Lakini baadae alinifuata tena na kubadili msimamo wake akitaka serikali mbili,” alisema Polepole.
Anasema kilichomshangaza zaidi kwa Lowassa ni pale alipopendekeza kuwa anataka muundo wa serikali mbili na kwamba serikali hizi mbili ziwe na uhusiano wa kijeshi pekee.
Akiendelea kutetea hoja yake ya kumpinga Lowassa, PolePole alisema kuwa amewahi kufanya kazi na Lowassa na kwa undani kabisa aligundua kuwa ni mbinafsi.
“Watanzania mnatakiwa kufahamu kuwa mnapokutana na Lowassa, Ninyi sio kitu bali kitu ni Lowassa,” alisema.
Mjadala huo ulitawaliwa na mivutano binafsi iliyowalazimisha kutoka nje ya mada mara kadhaa hususan baada ya Mchungaji Msigwa kutoa tuhuma za Polepole hadharani kisha akampa nafasi ya kujitetea.
Baada ya PolePole Kujitetea kufuatia tuhuma hizo, Mchungaji Msigwa alimueleza kuwa alichokifanya ndio kinaitwa ‘natural justice’ ambayo Edward Lowassa hakupewa wakati ule.
Akizijibu hoja za Polepole huku kukiwa na majibishano ya hapa na pale, Mchungaji Msigwa alikiri kuwa yeye ni mmoja kati ya wanachama wa Ukawa waliomsema sana Edward Lowassa na kumuita fisadi lakini sasa ameamua kukaa kimya.
“It’s true tulisema. Hata mimi nilisema, it’s true I can’t deny it. Lakini hata Joe Biden (Makomo wa pili wa Marekani) alikuwa anamsema Obama kuwa ‘he does not fit for Commander in Chief, lakini alipochaguliwa wakafanya kazi pamoja. Hatuwezi kusema kana kwamba Lowassa ndiye muovu kuliko mtanzania yeyote hapa nchini,” alisema.
Aliongeza kuwa kitu kikubwa alichojifunza kwa Lowassa na kumfanya amheshimu sana, ni moyo wa uvumilivu na kukaa kimya hata pale alipokuwa akitukanwa kila kona na kuitwa Fisadi. Alisema moyo huo wa uvumilivu hata watumishi wengi wa Mungu hawana.
Alifafanua kuwa katika ulimwengu wa siasa ni kawaida kufanya kazi na mwanasiasa ambaye awali ulikuwa ukimpinga sana kwa kuwa muda ukifika akaamua kubadilika mambo hubadilika pia.
Msigwa alisema kuwa chama chao ni chama cha demokrasia na maendeleo na kwamba hilo ndilo limewapelekea kumfungulia mlango Edward Lowassa baada ya kumhoji na kumuelewa.
Alipinga hoja ya Polepole kuwa Lowassa ana mapesa mengi ambayo ameyapata kwa njia zisizofahamika, Msingwa alisema kuwa maelezo hayo hutolewa bila kuelezewa kwa undani kama ana pesa nyingi kuliko nani (serikalini).
“Unasema Lowassa ana mapesa mengi, ni kama vile unajua akaunti zote za Lowassa zina shilingi ngapi. Na husema ana fedha nyingi kuliko nani?”
Aliwataka watanzania kutomchukulia Lowassa kama vile ndiye mtanzania mwenye dhambi nyingi kuliko wote bali wajikite katika kuangalia nia yake ya dhati ya kuleta mabadiliko ya kweli nchini.
Alisisitiza kuwa Chadema hawana muda wa kumsafisha Lowassa kwa kuwa umati uliofurika kumsindikiza kuchukua fomu ya kugombea urais katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Mkuu (NEC) inaonesha jinsi ambavyo watanzania wana Imani naye.
Alisema kuwa kwa mujibu wa tafiti zilizofanyika hivi karibuni zinaonesha kuwa ni asilimia 5 hadi 8 tu ya watanzania ambao wamejikita katika kufahamu ufisadi wa wagombea na kwamba umma mkubwa unataka mabadiliko kwa kuwa wamechoshwa na muundo.
Msigwa alimtaka PolePole kutomzungumzia Lowassa pekee kwa mtazamo hasi bali azungumzie pia ubaya wa Magufuli ambaye anaunga mkono muundo wa serikali mbili kinyume na ile anayoisapoti Polepole na Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba. Na kwamba yapo maovu mengi kwenye wizara ya ujenzi inayoongozwa na Mafuli.
Akijibu hoja ya Msigwa, PolePole alisema kuwa yeye ni mmoja kati ya watu walioishawishi CCM kukata majina ya wagombea wote wenye madoa katika mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea urais.
Alisisitiza kuwa ingawa CCM ni chama chake, hatampigia kampeni Magufuli hadi pale ambapo rufaa zilizokatwa dhidi ya wagombea waliotangazwa kuwa washindi wa kura za maoni ziangaliwe na wote wenye madoa waondolewe.
“Ili niwaunge mkono, CCM mnatakiwa kuwakata watu wote katika mchakato wa kura za maoni wanaotuhumiwa kwa kashfa mbalimbali,” alisema Polepole ambaye awali alitangaza kutembea nchi nzima kuhamasisha watu wasimchague Lowassa.
PolePole alitoa ushauri pia kwa chama chake cha CCM ili kiwe tofauti na makosa yaliyofanywa na wahasimu wao wa kisiasa, Ukawa.“Viongozi wa CCM, kama Ukawa wamewachukua watuhumiwa wamewakubali. Nyie onesheni uongozi na utofauti mhakikishe mnawakata wagombea wote wanaotuhumiwa. Onesheni kwamba watuhumiwa hawana nafasi kwenu.

14 comments:
HUYU JAMAA NDIE MIONGONI WALIOHONGWA KUTUHARIBIA KATIBA. LEO ANAKUWA WA KWANZA KUNYOOSHEA WENZIE VIDOLE ILHALI YEYE NDIYE AMETHIBITISHA UBINAFSI MKUBWA SANA.
Mti wenye matunda mazuri ndio hupigwa mawe. Kijana endelea na mawe yako. Uzi ule ule delete CCM
Ww polepole utakwenda pole pole hadi kuzimu
Hongera sana Bw. Humphrey Polepole kwa kutuamsha sisi wabongo tuliowajinga kwa kufuata mkumbo tusioujua. Nakumbuka maneneo ya mwalimu Nyerere aliyesema huu ni ushabiki mkubwa tusiojua, wamekatiwa hela nyingi akina Mbowe, Mbatia, Makaidi, Seif Sharif, Lissu, Msigwa na wengine viongozi wa UKAWA. Sisi wajinga tunafanya ushabiki tusioujua.
Nami sasa nakuunga mkono, pmaoja na jamaa zangu, ninakuahidi tuko pamoja tutazunguka wote Tanzania nzima kupinga na kuelimisha jamii juu ya HILI LIFISADI PAPA ( EDWARD LOWASSA). Hatuwezi kukubali nchi ikaenda mikononi mwa MAFISADI PAPA, akina Rostam Azizi, Karamagi, Msabaha, Vijisenti, Mbowe, Lisuu, Mbatia, Makaidi, na akina Msigwa. TUKO PAMOJA USIWE NA SHAKA BWANA POLEPOLE.
Nitahakikisaha ninawaelekeza na kuwapa vifungu wanasheria wa CCM, ili wamfungulie mashitaka kwa kosa la wizi wa mamilioni ya Richmod. Nitawaelekeza namna ya kuifanya kesi hii ya Richmond iende haraka na imalizike kabla ya Oktoba 25, 2015, ili safari ya matumaini iishie kwa kuwafuata akina Mramba na Yona huko waliko KEKO. Ndio itakuwa fudisho kwetu wabongo wapumbavu tunaoshabikia tusiyoyajua.
Ila hata akiachwa, hana ubavu wowote wa kupambana na Magufuli, kwa kila hali.
MUNGU ibariki Tanzania, na utuelekeze jinsi ya kupambanua mambo. Miaka yote tumekuwa tukilalamikia mafisadi, sasa leo tuwashangilia na kutaka wachukue nchi yetu, hii haiwezekani hata kidogo. Lowassa hana jipya anataka kuturudisha tulikotoka.
Muulize Lowassa, utaondoaje umaskini? kwa kuwa amekuwa akisema anataka kuondoa umaskini, ila hasemi ataondoaje umaskini.
Kama kawaida chochote cha ukweli kitakachozungumzwa juu ya lowasa utaona wahovyo jinsi wanavyohangaika kuupindisha ukweli. Lowasa ni fisadi tena wakuwepo lupango hayo si maneno ya CCM bali ni ya chadema. Lowasa ni fisadi ushahidi tunao wakimaandishi hayo sio maneno ya CCM bali ni ya uongozi wa chadema. Lowasa katika mapapa makuu ya ufisadi nnchini yeye ndie namba moja hayo sio maneno ya CCM bali ni ya chadema. Tena kwanini mnakuja kwa jazba vitu ambavyo ni vya ukweli kabisa kutokana na kauli zenu. Hata mkimiminika kuupinga huu ukweli kwa idadi ya mtoa maoni mmoja kwa mia moja bado watu wanakuoneni wapuuzi tu na ukweli utabakia pale pale .
Huyu mtu Polepole, mbona kashindwa hoja na kaonekana mkafiki mkubwa kinyume na inavyoandindikwa hapa? Huyu kijana hana maadili yeye mwenyewe na ni unafiki kuongelea maadili ambayo mwenyewe huna na una tuhuma za rushwa za ngono kama Msigwa alivyoeleza.
Jamani PolePole uwe makini sana...Politics is Dynamic...Mti wenye matunda siku zote ndege wa aina zote hutua pale... Thibitisheni huo ufisadi wa Lowassa...Mbona hakupelekwa Mahakamani? Je Lowassa alikuwa juu ya sheria? Angeshughulikiwa kama mtanzania... Mbona kina Andrew Chenge wapo mahakamani? Mara nyingi Lowassa amesema kuwa Rais wa nchi pia anahusika mbona hakuna laiyejitokeza kumpinga? Badala ya kumkubali Kiongozi mwnye dhamira safi mnamsimanga...Sisemi Magfuli hafai...Wote ni viongozi...tofauti ni Vision na Mission... Tulia Tafakari kabla ya kuongea Chochote....
Vichaa wa Chadema/Ukawa shangilieni, kweli Lowasa kawaloga vibaya hata vichwa vyenu havifanyi kazi, mnadhani ni mkombozi wenu? Kumbe kawapora chama chenu. Inabidi mpige bao na mpate miti shamba kuponyeshwa akili zetu...poleeni, Fisadi keshawaweka mikononi mwake. Ukawa/Chadema itakuwa the new breeding ground ya MAFISADI maana mmepata the perfect sire!
watatapatapa na wataongea ngonjera zote lakini mwisho wa siku CCM lazima ipigwe chini huu ni mwaka wa mabadiliko. Tumewachoka CCM na kurithishana madaraka ukoo kwa ukoo.. watanzania wa leo sio wa 47 , wanaona na kusikia...
mimi nawashangaa sana wana siasa siku zote ni watu wanao dhania sisi wengine tunao jishughulisha na kazi nyingine huwa ni wehu, kuna ubaya gani mimi ikiwa nataka kiongozi nilie mchagua hata akiwa jambazi?
Nafikiri huu ni uamuzi wangu na wewe kama una taka kiongozi mwenye sura nzuri au kasisi chagua huku katazwa na mtu sasa kwa nini tuna lazimishana au tuna chaguliana wa kutuongoza?
Bwana Polepole mimi nina haraka na maendeleo ya nchi hii, ndio maana nimeamua kumuunga mkono Lowassa anae chukia umasikini kama ukoma.Wewe na wenzio kumbatieni umasikini huo pia ni uhuru na uamuzi wetu ikiwa Lowassa ni fisadi basi nchi hii hasa viongozi wa ccm wengi hawato salimika na nembo hii nafikiri unajua kuwa kuna waliojiuzia migodi,mabenki,majumba na kujikopesha mabillioni hao wote bado ni viongozi wa ccm wengine wamestaafu lakini wao ndio wanao amua wagombea wa chama hicho sasa uamuzi wa kumtukana Lowassa na kumbebesha mzigo mzito wa ufisadi peke yake wakati wengine unawajua uwezo huo kakupa nani?
WENGINE TUTAENDELEA KUMUUNGA MKONO LOWASSA NA NYIE ENDELEENI KUIMBA NYIMBO YENU YA TAIFA LA UFISADI HAMJAKATAZWA,MUHIMU MKUMBUKE TU AKIJA AKITOKA MHESHIMIWA MWINGINE CCM ITABIDI PIA MUINUKE NA KUENDELEA KUMUIMBIA WIMBO HUO HUO, KWA SABABU NDANI YA CCM WASAFI WAMEKWISHA TANGU ENZI ZA MWALIMU NDIO MAANA WANAKUJA 'UKAWA' TUWASAFISHE UPYA.
MDAU.
ILALA.
TUSEME UKWELI HIVI UFISADI WA LOWASSA NI UPI?? RICHMOND KAHUSIKA KIKWETE TANGU KIKAO CC KILICHOKETI DODOMA MWAKA 2011 KILA MMOJA WETU ANAJUA KUWA KIKWETE NDIYE MHUSIKA MKUU...INAWEZEKANA VIPI MRADI UPITISHWE BILA KUPATA BARAKA YA JUU???? NCHI YETU HAIONGOZWI NA WAZIRI MKUU BALI NA RAIS NA KINACHOTOKEA RAIS WA NCHI ANAKUWA RESPONSIBLE....HATA ESCROW HAKUHUSIKA WEREMA, MUHONGO AU MWINGINE YULE, MUHUSIKA MKUU NI RAIS KIKWETE NDIYO MAANA BARUA ILIANDIKWA NA IKULU KUACHILIA (TO RELEASE THE MONEY)PESA. TUSIWALAUMU MAWAZIRI WAO HAWANA MAKOSA...MWENYE MAKOSA NI MKUBWA WA JUU KABISA KWANI HAKUNA LINALOPITA AU LILILOPITA BILA YEYE KUFAHAMU NA KUIDHINISHA, TUWE NA UFAHAMU WA KUELEWA....SAINI YA MWISHO KWENYE HIZO PROJECTS NI YA NANI????? SIJAWAHI KUSIKIA HAO WANAOSEMA LOWASSA FISADI WAKISEMA ANA KIASI GANI CHA FEDHA....HAYUPO KWENYE FEDHA ZA USWISI, HAYUPO KWENYE KASHFA YA RADAR, HAYUPO KWENYE KASHFA YA MIGODI YA KIWIRA etc etc SASA YUPO WAPI?????
Anachosema huyu jamaa kinalingana na serikali ya CCM huko nyuma kumuita kaburu mtu mbaya sana. Leo hii kaburu ndiye mwekezaji kwenye madini, gesi nk. Ari yetu ni moja " Toa CCM ikulu ingia Ukawa"
Chama gani kinachotaka kutawala milele?ccm they're very selfish,tunachongojea ni lowassa kuapishwa tu,
Acheni watanzania waamue sio wajinga
Post a Comment