Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).
Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:
(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).
(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa
Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico.
(iii) Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015


1 comment:
LAKINI KWA NINI UBALOZI MAREKANI TENA AWE MHAYA (MTU WA KAGERA)? HAKUNA WATANZANIA MAKABILA MENGINE (MIKOA MINGINE) WENYE UTASHI NA UWEZO WA KUIWAKILISHA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA? INASIKITISHA KUONA UPENDELEO WA HALI YA JUU KATIKA SUALA LA UTEUZI WA BALOZI MAREKANI, KWANI ALIYEONDOKA NA ANAYEKUJA WOTE NI KABILA MOJA (WAHAYA) KITU AMBACHO MH.HAYATI NYERERE, MH. MWINYI, NA MH. MKAPA NINA UHAKIKA WASINGEFANYA HIVYO. YAELEKEA KUNA TATIZO KWENYE WIZARA YA MAMBO YA NJE, UKABILA LAZIMA UKOMESHWE. TUNAMUOMBA MH. MAGUFULI AJE NA FAGIO KUBWA KUSAFISHA WIZARA NA MABALOZI WANAOTUWAKILISHA, WE WANT A FAIR PLAYING FIELD, NI TANZANIA YETU SOTE. TAFADHALI DJ LUKE USIBANE HILI, NAJUA BLOGU YAKO NI MOUTH-PIECE YA UBALOZI WASHINGTON, USA. ASANTE.
Post a Comment