Ni asubuhi tulivu kabisa ya Jumatatu tarehe 10/8/2015.Ni siku ya kihistoria katika Taifa letu.Hii ni kwa sababu Kamanda mpambanaji na asiyechoka mzee wa Maamuzi magumu Edward Ngoyai Lowassa akiwa na mgombea mwenza Juma Duni Haji watachukua rasmi fomu za kugombea Urais kupitia UKAWA katika ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Timu ya wanahabari wa JF tayari iko hapa buguruni katika ofisi kuu za CUF ili kuwaletea kila kitakachojiri.Tunatarajia maanadamano haya makubwa yataanza saa 3 asubuhi hapa ofisi za CUF na yatapitia katika ofisi za NCCR Ilala na kisha baada ya kuchukua fomu maanadamano haya yatendelea mpaka kumalizikia ofisi za CHADEMA Kinondoni.
Tunatarajia Edward Lowassa kusindikizwa na waendesha baiskeli,bodaboda,maguta,bajaj i,magari na pia tayari tuna taarifa za idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo vikuu DSM kushiriki maandamano hayo.Pia watakuwepo akina mama Ntilie (mama lishe),wamachinga na wale wote watakaoguswa kushiriki tukio hili la kihistoria.

No comments:
Post a Comment