ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 25, 2015

MAMA SAMIA SULUHU ALITEKA JIMBO LA MOSHI MJINI LEO AGOSTI 25, 2015

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM Mama Samia Suluhu akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wake wa kampeni aliofanya kwenye Viwanja vya CCM Majengo, jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, leo Agosti 25, 2015. (Picha na Bashir Nkoromo).
Wananachi wakimpongeza mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya CCM Majengo jimbo la Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro leo, Agosti 25, 2015
Sehemu ya wananchi wakimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Agosti 25, 2015, mjini Moshi.
Mwananchi akimshangilia kwa nguvu na hisia kali, mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Agosti 25, 2015, mjini Moshi
  Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akishiriki kucheza ngoma, kundi la kina mama wa mjini Moshi lilipokuwa likitumbuiza wakati wa mkutano huo wa kampeni jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, leo Agosti 25, 2015
Aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo la Nkenge mkoani Kagera, Adupta Mshanga, akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano huo, leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akimpongeza kwa hotuba nzuri mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Moshi Mjini, Davis Mosha, wakati wa mkutano huo uliofanyika katika jimbo hilo mkoani Kilimanjaro,leo Agosti 25, 2015.
 .Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Tanga, Ummy Mwalimu akimuombea kura mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli wakati wa mkutano huo, leo Agosti 25, 2015
Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kizigha akimkaribisha kuzungumza,Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia wakati wa mkutano huo.
Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwanadi wagombea wa Ubunge, Davis Mosha (Moshi Mjini), Innocent Meleck (Vunjo) na Dk. Siril Chami (Moshi Vijijini) wakati wa mkutano huo.
Kamanda wa UVCCM wilaya ya Kinondoni, Agela Kairuki akimshauri jambo, Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama samia wakati wa mkutano huo.
Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akizitazama vema picha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Raishid Kawawa, alizozwadiwa na mchoraji huyo maarufu wa mjini Moshi, Omari Mwariko (65), wakati wa mkutano huo.

No comments: