ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 12, 2015

MBONA NI KAZI KIDOGO TU ILI MH LOWASSA ASIWE FISADI AU MWIZI,

1- Chadema wajitokeze mbele waseme wao ni wadanganyifu na Matapeli wa kisiasa.
2- UKAWA wajitokeze na kusema ni kikundi cha walinda MAFISADI na sio wanao pambana na UFISADI.
3- Chadema wajitokeze na kusema katika ile RIST OF SHAME ya watu 11 akiwemo na LOWASSA waliandika wakiwa WAMELEWA.
4-UKAWA wajitokeze watwambie lini wameamua kuunga mkono serikali mbili za bwana LOWASSA.
5- UKAWA wajitokeze watwambie wamejua ni kiasi gani cha Mapesa alichotumia LOWASSA wakati wa kusaka urais ndani ya CCM na kiasi gani atatumia UKAWA.
6- UKAWA wajitokeze na watwambie wanawajua hao marafiki wa LOWASSA wanaompaga Mapesa na kwa masharti gani.
ASANYENI NAOMBA MAJIBU WANAUKAWA WOTE.
MWISHO Namkumbusha Maalim Seif niliwahi sikia sauti toka kwa mwana mama wa CCM wakati wa Bunge la katiba akisema hawata toa nchi kwa vikaratasi.
TWENDENI TUKAFYEKE MAPORI.
 David Maphone katika ubora wake miaka 800

19 comments:

Anonymous said...

HOJA NYINGINE BWANA UTAFIKIRI MTOA HOJA KALEWA CHANG'AA...ANY WAY NDIO WATANZANIA HAO, NA NDIO HUMU HUMU TUNACHAGUA VIONGOZI.. SITOSHANGAA KAMA MIFUMO HII MIBOVU ITAENDELEA SIKU HADI SIKU, NAAM, WALIMU WABOVU, SHULE HAKUNA MADAWATI, WIZI WA MITIHANI, UPENDELEO, WATOTO WA WAKUBWA KUENEDLEA KUNUFAIKA, WAZAZI KUKOSA MAHALI PA KULALA MAHOSPITALINI. HALI HIZI NA NYINGINE NYINGI KAMWE HAZITOBADILIKA KWASABABU, FIKRA ZETU BADO NI ZILE ZILE, TUNAACHA MADA ZINAZOTATIZA WADANGANYIKA, TUNAMG'ANG'ANIA MGOMBEA KWA LAWAMA. TUNAACHA KUJADILI RUSHWA KEDE KEDE TUNGANG'ANG'ANIA RICHMONDI, VIPI ESCROW?JE EPA?...TUNAWEXA KUZITAJA NA KUZITAJA PASI KUMALIZA ILA KWA FOCUS YETU FINYU TUNAENDELEA KUNYOOSHA KIDOLE KWA MTU MMOJA ILHALI KUNDI KUBWA LIKO UPANDE WAPILI NA LINAENDELEZA LIBENEKE...ALAMSIKI WAUNGWANA TUTACHORA SANA MWISHOWASIKU TUNAUZIWA PICHA, YA MAGUFULI HUKU NYUMA YAMEJIFICHA MAJITU YALE YALE...

Anonymous said...

Alishasema fisadi ni Nani

Anonymous said...

Nyinyi Ccm mmezidi kutapatapa kama jahazi linazama ogeleeni mje Ukawa, kila kukicha Lowasa wakati ccm ni mafisadi watupu hakuna hata mmoja mwenyeafathali. Wewe angalia Escrow, issue ya waswis kkukamata meno ya tembo kutokea Dar halaafu mnathubutu kumwita Lowasa fisadi kwa issue ambayo ilikuwa ya mtawala wenu wenyewe. Kweli hao wahenga waliposema nyani haoni kundule hawakukosea

Anonymous said...

Well said, it's time for change!!! CCM HAMNA SERA KABISA, WIZI MTUPU, WATU WANAHANGAIKA , WATOTO HAWANA WALIMU MASHULENI ALAFU MIJITU INACHOTA TUU, PUMBAVU, PITISHA URAI PACHA HAPO TUJE KUWAFUNDISHA JINSI YA KUWAJIBIKA.

Anonymous said...

Kweli kabisa CCM hamna sera !!!

Anonymous said...

Haniingilii kichwani eti watu wanakutwa na shahada nyingi za kupiga kura
Jamani si kuna alama za vidole kila kadi
Au ndo goli mkono
2015 mwakaaa huu Hampati NGO

Anonymous said...

1 USD = 101.25 Kenyan Shilling.
1 USD = 727.58 Rwandan Franc.
1 USD = 2,117.95 Tanzanian Shilling.

Sasa kweli TUTAFIKA???..halafu kuna watu bado wanashabikia serikali ya CCM!! hivi WATANZANIA TUMELAANIWA AU VIPI? kuwa masikini siyo sifa!! Kuishi bila kupata mahitaji muhimu siyo sifa!! Amkeni jamani!

Anonymous said...

Huko ccm mbona majizi yamejaa tele kwa nini usianze kuya judge huko?au ndio siasa hizo?mbona kiongozi wa nchi alihusika humzungumzii?kama imekuuma sana lowasa kwenda UKAWA itabidi ule malimao debe,mwisho wa siku wananchi ndio watakaoamua.

Anonymous said...

Waalimu tunahitaji mikopo ya nyumba na si Laptop
Magufuli uumeuza nyumba za serikali kwa bei Chee ukiingia ikulu utauza kila jk alingia kwa vishindo a anaondoka kimya kimya
Watanzania hawali barabara
Wanahitaji chakula, afya, elimu
Na ulivhofanya hata kipofu angefanya
Na ufisadi ujenzi hakuna

Anonymous said...

kitu kimojaa ukawa wajue lowassa siyo chadema wala ukawa akiwa raisi mtakuja kulijua hilo.lowassa ni ccm mtake msitake.na msipo angalia lichama lenu litakuja kuchujaa na kufaa kama ilivyokuwa Enzi za mrema na nccr mageuzi yake.yupo wapi sasa hivi choka ile mbaya.

mnawakaribisha watu kwenye vyama vyenu hajawasoma hajui mbinu zao.kalaga bao. professa wa kinyamwezi kakimbia na mbinu zote za uchumi wa cuf mmebaki macho juuu.

mtaisoma number na mjua nani bala la siasa.wanafukuzwa kiaina aina na si kweli ili muwapoke halafu INAKULA KWENU.

mtakuja kuniambia kuna siku mtakuja kuniambia hapa hapa.

ccm si mchezo mtaisoma number.

tafuta kula yako na mkeo na wanao politics is a dirty game.shauri zenu.ushabiki maandazi wa kijuha juha mtaku kostini sana.wenzenu wana fanya yao nyinyi mnashabikia tu bila kujua njia wanazo zitumia.

Anonymous said...

Ubishi ni wa nini tena mdau #1 and #3? Mdau #1 anazungumzia watoto wa wakubwa wanaendelea kunufaika. Hiyo ni kweli kwani huyu Fisadi mliyempokea na kumpa chama chenu anaye mtoto mwenye mansion pale Uingereza, jee? unadhani akishinda atawapeleka watoto zenu na kuwanunulia hayo manyumba pia? Ukweli ni kwamba,huyu jamaa hajikuwakomboa, face it folks, bali anakuja kujinufaisha tuu, kama atabahatika kuchaguliwa. Mdau #3, sielewi kama nawe umepoteza akili kama wengi ukawa walivyokumbwa. Huoni ni aibu kwa viongozi wa Ukawa ambao walikuwa wanapiga kelele usiku na mchana kujishushia hadhi na kumruhusu Fisadi to dictate for them? Are all Ukawa leaders that stupid? Walisema, eti wao tuu ndo wataleta mabadiliko, yet they are so weak to take control of their parties destiny that a disgraced CCM reject comes to their rescue? That is what we call inferiority complex, and is well displayed by Ukawa leaders. Sasa tuambieni mtafanya nini after October akishindwa? Mtamfukuza na kuwarudisha akina Lipumba na Slaa? Poleeni, kwa vuruga litakalolipa Ukawa baada ya Oktoba.

Anonymous said...

Waliolewa Chang'aa hapa leo wapo wengi tena chakari wakati mtu analaumu mifumo mibovu kwani huyo lowasa atokana na mifumo gani?, aah sijui hakuna madawati, sijui walimu wabovu, sijui wizi wa mitihani, aah rushwa kede kede yaani vile vile kilevi kilevi hata point ya hoja huioni iko wapi. Sasa nauliza hivi tafadhali msinikatishe suala langu mpaka nimalize kuuliza. Ni hivi kama sio rushwa lowasa na Dr slaa nani alistahiki kuwa mgombea wa ukawa? Kama sio rushwa kitu gani kilichozuia kupatika mgombea wa ukawa kwa njia ya kidemokrasia na kina lipumba na dk slaa na wao wakaenguliwa kwa njia ya haki? Kama sio rushwa iliotumika kuwaziba midomo na akili baadhi ya viongizi wa ukawa, tangulini lowasa akawa msafi wa ufisadi? Ikiwa mgombea wa uraisi katoa rushwa ili apitishwe kugombea uraisi jamani huyo mtu akija kuwa raisi hiyo serikali itakuwa ya aina gani? Jamani hao wanaowaita makukuru sijui takukukuru wanakazi gani kwanini wasiichunguze hii rushwa ya wazi wazi kwa nini wasiende kumuhoji dk slaa kulikoni? Au hao takukuru walikuwa chini ya lowasa moja katika mitandao yake? Mtoa mada kuu ya hapo juu katoa nasaa za msingi kabisa sasa wenye hoja wazijibu sio muanze kuropokwa hovyo kama Tundu Lisu. Any way thanks for whoever create this blog it has been real helpful in exchanging ideas as well as news information and more concerning our culture . It is just like someone inviting you for a meal and then after stuffing your stomach getting up and go no thanks nothing kind shameful thing to do. So again thanks for your service and hopefully will keep it going . I know you hear the complains some people say you're CCM spoiled brat and others say you're no different as Mr mbowe and ukawa . For me i think the way i see tings have been balancing fairly just keep it on.

Anonymous said...

Kwa hiyo CCM mnataka kutwambia kwamba tukiweka mtu safi ndo tutashinda? Mnatupa advise, sio? Kwanza mtueleze kama meno ya Tembo aliyaiba Lowassa, aliyepeleka wanyama kwenye ndege ni Lowassa, ESCROW inamhusu Lowassa, D. Ulimboka alipigwa na Lowassa, nyumba za serikali ziliuzwa na Lowassa. Mkishaeleza hayo, tutawasikiliza.

Anonymous said...

Ccm why don't u mind your own business,mnaacha kukaa kumzungumzia msafi makufuli mnakaa kumzungumzia mtu ambae hawahusu,kweli yamewafika.Na bado sana.

Anonymous said...

Umekunywa viroba wewe nenda zako wala hutambui uko wapi

Anonymous said...

NAAM, TATIZO NI MIFUMO, NDIO INAZAA RUSHWA NA KUTOTHAMINI WENGINE, SASA SWALI NI NANI ALIYEJENGA MFUMO HUU? JIBU NI CCM, WALE AMBAO WANAKUWEKEA PICHA YA MAGUFULI HUKU NYUMA WAMEWAFICHA AKINA CHENGEI, NA KUNDI LA WALA RUSHWA WENGINE WEEENGI. NA KWA KUWA UWEZO WAKO NI MDOGO WA KUELEWA SANAA HII, UNANG'ANG'ANIA PICHA YA MAGUFULI. KUMBUKA MAGUFULI ANAENDELEZA SERA ZILE ZILE. KWA SISI WENYE BUSARA TUNAANGALIA NYUMA YA LOWASSA NA MAGUFULI KUNA NINI, NA NDIO TUNACHAGUA.SASA WEWE USIJESTAAJABIKA UTAKAPOGUNDUA KUWA YALE YALE MAJAMAA YALIYOKUUMIZA YANARUDI MBELE MARA BAADA YA UCHAGUZI...USITEGEMEE MAPYA KWA WATU WALE WALE, MFUMO ULE ULE, SERA ZILE ZILE,MIPANGO ILE ILE YA KUISOMA NAMBA. KUMBUKA HUU SIO USHABIKI WA MPIRA HAKUNA DERIVATIVE KWENYE SIASA, SIASA NI HALI HALISI, NA UTACHAKOAMUA SASA NDICHO KITAKUFUATA SIKU ZOTE. CCM TIUJIBU HOJA NA SI KUKASHIFU WATU, TUAMBIENI MTAFANYA NINI SASA BAADA YA MIAKA HAMSINI...MTAFANYA NINI KUONDOA RUSHWA ILIYOKITHIRI, TUACHE SANAA ZA KUNG'ANG'ANIA MAMBO RAHISI RAHISI YA KUNYOOSHEA VIDOLE MTU.

Anonymous said...

Wewe nimeshakuambia mara kadhaa kuwa uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo sana. Unabwabwaja tu!

Kimsingi, CDM imeshakuwa CCM daraja la pili. Huwezi ukabadilisha mfumo fulani kwa kutumia watu wale wale waliokuwa vinara kwenye mfumo ambao unadai ni mbovu na unahitaji kubadilishwa. Hao mafisadi wanahamia CDM baada ya kukosa fursa ya kuendelea kufanya ufisadi wao ndani ya CCM. Wanahamia CDM kutafuta fursa ya kujaribu tena bahati ya kuendelea na shughuli zao haramu. Hao firauni si tu hawajui sera zozote za CDM, lakini pia hawaijui hata Katiba ya CDM.

Kama una brain inayofanya kazi ipasavyo, huwezi ukaichukia CCM halafu ukaipenda CDM ambayo inatumia wachezaji wa CCM. Kwa hali ilivyo sasa hivi ndani ya CDM, wachezaji ni walewale wa CCM isipokuwa wamevaa jezi tofauti. Kama wachezaji walikuwa wabovu ndani ya CCM, hawawezi kuwa wazuri ndani ya CDM eti tu kwa sababu wamevaa jezi tofauti!

Anonymous said...

Wewe nimeshakuambia mara kadhaa kuwa uwezo wako wa kujenga hoja ni mdogo sana. Unabwabwaja tu!

Kimsingi, CDM imeshakuwa CCM daraja la pili. Huwezi ukabadilisha mfumo fulani kwa kutumia watu wale wale waliokuwa vinara kwenye mfumo ambao unadai ni mbovu na unahitaji kubadilishwa. Hao mafisadi wanahamia CDM baada ya kukosa fursa ya kuendelea kufanya ufisadi wao ndani ya CCM. Wanahamia CDM kutafuta fursa ya kujaribu tena bahati ya kuendelea na shughuli zao haramu. Hao firauni si tu hawajui sera zozote za CDM, lakini pia hawaijui hata Katiba ya CDM.

Kama una brain inayofanya kazi ipasavyo, huwezi ukaichukia CCM halafu ukaipenda CDM ambayo inatumia wachezaji wa CCM. Kwa hali ilivyo sasa hivi ndani ya CDM, wachezaji ni walewale wa CCM isipokuwa wamevaa jezi tofauti. Kama wachezaji walikuwa wabovu ndani ya CCM, hawawezi kuwa wazuri ndani ya CDM eti tu kwa sababu wamevaa jezi tofauti!

Anonymous said...

Anachosema huyu jamaa kinalingana na serikali ya CCM huko nyuma kumuita kaburu mtu mbaya sana. Leo hii kaburu ndiye mwekezaji kwenye madini, gesi nk. Ari yetu ni moja " Toa CCM ikulu ingia Ukawa"