Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru. Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumer Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu . Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza, Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini. Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu, Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai. Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini. Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai. Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini. Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini. Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.
Na Joachim Mushi, Arusha CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana. Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine. Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini. "...Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya...hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku," alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu. Alisema Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha 'General Tyre' ikiwa ni mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana. Aidha alisema mpango mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, "...Tukifanikiwa kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari madogo na makubwa," alisema Bi. Suluhu. Aliongeza Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka. Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo. Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana.
5 comments:
Acheni uongo mgambo ni jeshi la CCM wanafanya Kazi kwa maagizo ya viongozi wa CCM
Samia hebu acha kuwagilibu waTanzania. Yaani sasa hivi hizo ilani za chama mlizojiwekea za kutudanganya kuboresha ajira kwa madereva sijui kuhakikisha dawa zinapatikana kwani huku nyuma hayonyalikuwa hayawezekaniki. Leo ndi mnakuja na haya. Hebu mngekuwa wa faida kwetu mngelitueleza hatima ya kitita cha ESCROW na pembe za ndovu zilizopita uwanja wa JK haiwezekaniki serikali unayoipigia debe imefanya madudu fulani hutuelezi ukweli!? Mnajifunga jukwaani.kuendelea kuwaziba macho waTanzania sio wakati huu bora ukweli ueleweke. Kwa nini mnakuwa kimya???
Hii kauli ya kuwainua kina mama na vijana haikuanzia kwako na hizo milioni 50 zipo wapi wakati halininazidi kituwia ngumu kila kukicha tukihangaika na biashara zisizolipa.
Mbona ahadi zimekuwa nyingi na za pesa kibao maelfu kwa mamilioni. Je yale ya ESCROW yamerejeshwa. Yaani hii inakuwa kama kiini macho kwani kila mkutano lazima kunawekewa ahadi za fedha maendelei maji kina mama, vijana wapi walikuwa siku zote jamani hii danhanya toto naa hizi Tshirt, kanga na madela mlogawa bure! Huu sio wakati muafaka wa kudanganya totos!!
Hahahaaa mkikubaliana na ahadi za ccm imekula tena kwenu kwa mara nyingine. Wimbo ni uleule wamebadilisha tuu mwimbaji
Post a Comment