ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 25, 2015

MGOMBEA URAIS DR MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA KAMPENI RUVUMA KUANZIA AUGUST 30


Picha kutoka maktaba

MGOMBEA Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dr. John Magufuli anatarajiwa kupokelewa na mamia ya wananchi wakiwemo wanachama wa chama cha mapinduzi katika kijiji cha Igawisenga wilayani Songea mkoa wa Ruvuma akitokea mkoa wa Njombe  tayari kuanza kampeni mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama cha mapinduuzi mkoani Ruvuma Mwenyekiti wa  kamati ya maandilizi ya kampeni mkoani Ruvuma ya mgombea uraisi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani Ramadhani Kayombo alisema kuwa Dr. Magufuli na msafara wake unatarajiwa kupokelewa Agost 30 mwaka huu majira ya asubuhi huko katika kijiji cha Igawisenga.
Kayombo alieleza kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani wanafanyiwa kampeni za kistaarabu katika kipindi chote cha kampeni ambapo mgombea uraisi Dr. Magufuli anatalajia kufanya ziara za kampeni katika wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru ambako atamaliza ziara septemba 02 mwaka huu na kuendelea na ziara mkoani Mtwara.
Alisema kwa kuwa wananchi wengi wana imani na chama cha mapinduzi ambao wanahitaji kumuona na kumsikiliza  hivyo amewataka wajitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni itakayofanyika wakati Dr. Magufuli akiwa mkoani Ruvuma na amewaomba kuwa na mshikamano wa pamoja katika kuhakikisha kuwa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu kinapata ushindi wa kishindo kwa mgombea uraisi, wabunge na madiwani na si vinginevyo.
 Na Jamvi la Habari Songea 
Kaimu Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketansi akizungumza na wanahabari(hawako pichani) juu ya Kampeni ya uhamasishaji wa utalii wa ndani kwa wazawa itakayodumu kwa muda wa miezi sita.

Baadhi ya Maofisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii wakizungumza na wanahabari (hawako pichani ) juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa ambapo katika kipindi cha miezi sita watakao tembelea zaidi ya Hifadhi nne watapata ofa ya kutembelea Serengeti ikiwa ni pamoja na kugharamiwa maradhi katika hoteli yenye hadhi ya nyota tano.
Kaimu Meneja Mauzo wa TANAPA,Victor Ketansi akisisitiza jambo.

Mkuu wa Idara ya Utali katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro,Eva Mallya akizungumza vivutio mbalimbali vunavyopatikana katika hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro.

Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni afisa utalii mfawidhi na mkuu wa kanda ya utalii Kaskazini,Lauriano Munishi akizungumza jambo mbele ya wanahabari(hawako pichani)juu ya uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha utali wa ndani.
Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha,(ANAPA) Neema Philip akizungumzia vivutio mbalimbali vinayopatikana katika hifadhi ya Arusha.
Afisa Utalii Mwandamizi katika Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi ,Pellagy Marandu akizungumzia vivutio mbalimbali vinavyoopatikana katika hifadhi hiyo.
Meneja Mawasiliano Mwandamizi wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Catherine Mbena akiwa na mwandishi wa habari wa TBC Kilimanjaro,Sauda Shimbo wakati wa kikao cha maofisa wa TANAPA na wanahabari kuzungumzia juu ya kampeni ya kuhamasisha wananchi kutembelea hifadhi za taifa .

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini..

No comments: