ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 25, 2015

LOWASSA, DUNI WATEMBELEA MASOKO YA TANDALE NA TANDIKA JIJINI DAR

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Wazee wa Tandale, wakati alipotembelea Soko la Tandale, jijini Dar es salaam leo, akiambatana na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni (kushoto).PICHA ZOTE NA MTAA KWA MTAA BLOG
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni  wakipata maelezo kutoka kwa Bw.Omari Juma (kulia) ambaye ni mfanyabiashara ya kuuza Maharage katika Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, wakati walipotembelea Soko hilo kujionea hali ya biashara masokoni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakiwapungia wananchi wa Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kijana ambaye ni muendesha baiskeli ya miguu mitatu (guta) aliekuwa akitoka kwenye Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi Mkubwa (jina lake halikupatikana kwa haraka) aliekutana nae ndani ya Soko la Tandale, Manzese Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipata kikombe cha chai ya maziwa iliyokuwa ikiuzwa na Mwanadada (jina lake halikupatikana mara moja) wakati alipotembelea soko la Tandale, Manzese, jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wananchi wa Tandale, Manzese, jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015, baada ya kutembelea Soko hilo.
Umati wa watu ukiwa umefurika nje ya Soko la Tandika, Temeke jijini Dar es salaam kutaka muwaona Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, waliotembelea Soko hilo leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakitembelea Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Kijana Alex aliekuwa akiuza maji ya kwenye vifuko vya plastiki, akizungumza jambo na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, wakati walipotembelea Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakikata mitaa ya Soko la Tandika, Temeke Jijini Dar es salaam leo Agosti 25, 2015.
Vijana wa Tandika wakiwashangilia Wagombea hao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwaaga wananchi wa Tandika.

6 comments:

Anonymous said...

Waswahili husema "Chema chajiuza, kibaya chajitembeza". Ulikuwa wapi muda wote ati leo kwa ajili unataka kura zao ndio unachitembeza na kujidai kuwatambua kuwa kuna walalahoi, akina mamantilie, wauza bidhaa sokoni na waendesha daladala! Wacha dharau yako. Hawa wote wanahitaji heshima zao kama binaadamu wengine na sio manamba tu wa kutumia wakati wa kutafuta ulaji wako.

Anonymous said...

Kwa nini asituletee angalau ng'ombe 1,000 kati ya zile 8,000 alizonazo kule Monduli, awakabidhi wachinjaji na kugawa nyama kwa walalahoi wanaokula sembe na maharage kila siku? Thubutu, hiyo tembezi yake ni feki tupu!

Anonymous said...

It's unfortunate hawa wafuasi wa ccm hawawezi kutoa maoni yao kiustaarabu au civil. Asilimia 99.9 ya maoni yao yametawaliwa either na chuki, wivu, na hasira. Mimi sioni tafauti na baba yao Mkapa kuwaita wananchi wenzake wapumbavu na malofa. Huo sio ustaarabu wakati wa kutoa maoni. Na utashangaa hawa wanaotoa maoni kama haya wanajiita ni wasomi. Ustaarabu hauuzwi na wala haununuliwi. Punguzeni hasira, chuki na wivu kwani hausaidii kitu.

Anonymous said...

Agadhali huyo kawajali. Wale walioiba mpaka tembo wamekaluzika umewaambia nini? Yaani viongozi wanagawana pesa za walipa kodi kwenye magunia mnajifanya mmesahau? Wao wanatibiwa India wewe unatibiwa wapi?

Anonymous said...

Mdau wakwanza acha chuki kama Lowasa ni chaguo la wanyonge atakuwa raisi tuu hata ccm mfanye nini pia atawasaidia zaidi na hiyo gesi iliyopatikana huko kwenu kuliko ccm walivyowafanyia na uache kusema anachitembeza nini bwana chinga

Anonymous said...

Mdau wa August 25, 2015 at 10:16 PM Nakushukuru kwa ujumbe wako na masahihisho yako. Nilivyoandika "unachitembeza" nilikuwa nakusudio la kuandika "unajitembeza" lakini kalamu iliteleza. Hata hivyo nashukuru uliona na kuelewa ingawa hukuliona la 7:15 PM hapo juu pale mwenzetu aliandika "Agadhali" akiimanisha "Afadhali". Hata hivyo shukurani sana sisi wote ni Watanzania na hoja zetu zote tunazoziandika hapa ni kwa ajili ya upendo wa nchi yetu na nia yetu ya kutaka tupate viongozi watakao lisukuma mbele gurudumu la maendeleo yetu wote. Pili, mimi si mmachinga na wala sina chuki na Lowassa wala kiongozi yeyote wa chama chochote ila sipendi kuona kejeli zinazofanywa na wanasiasa hasa wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi. Wacha viongozi wetu waende kujinadi kwa wananchi bila kuvaa ngozi ya kondoo hali wakiwa ni chui. Kupanda daladala au kuzunguka sokoni leo ati unakwenda kuangalia kero za wanyonge wakati miaka yote iliyopita hujawahi kufanya hivyo kama sio kuwadhalilisha hau unaokwenda kuwaona ni nini? Mungu Ibariki Tanzania yetu na nitamkubali kiongozi yeyote atakayechaguliwa na wengi kwa niaba yetu tulioko huku Ughaibuni.