ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 17, 2015

MKUTANO KATI YA SERIKALI YA TANZANIA NA YA JAPANI JUU YA MIRADI YA MAENDELEO

Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (aliyesimama) akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto kwake ni Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango. Wengine ni Bibi Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa kwanza kulia), Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa tatu kulia). Picha na maelezo na Thomas Nyindo Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango
Ujumbe kutoka Serikali ya Japan ambao unajumuisha Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan wakifuatilia mjadala kwa makini.
Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe huo Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania (wa pili kushoto) akisistiza jambo wakati wa mkutano huo. Wengine pamoja nae ni wajumbe kutoka Serikali ya Japan.
Wajumbe wakifuatilia majadiliano hayo kwa umakini yatari kwa kutoa michango yao juu ya mada iliyoko mezani.

Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pamoja na majukumu mengine, inajukumu pia la kuratibu miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa serikali ya Japan kila mwaka. Maandalizi ya mwaka huu yameshakamilika na mkutano wa majadiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania na Serikali ya Japan ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hotel ya Hyatt Regeny, The Kilimanjaro, Dar es Salaam. Majadiliano hayo kwa upande wa Serikali ya Japan yaliongozwa na Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania, kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Malengo ya mkutano huo ni kujua hatua iliyofikiwa katika maombi ya ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka Serikali ya Japan kwa mwaka 2014/15, kuwasilisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili kwa mwaka 2015/16, kujadiliana changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuboresha ushirikiano baina ya Serikali hizi mbili. Pia Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, iliwasilisha mawazo ya awali ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II).

Wizara zilizoshiriki katika Mkutano huo ni pamoja na Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Wizara ya Fedha.

Wizara zingine ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Mendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, na Tume ya Mipango – Zanzibar.

Kwa upande wa Serikali ya Japani taasisi zilizohudhuria ni pamoja na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan.

No comments: