Taasiisi ya FRIENDS OF DEVELOPMENT (FOD) Inategamea kufanya mkutano wake katika viwanja vya leaders kwa kuwa kutambulisha viongozi wa dar es salaam na kusajili wanachama wapya,
zoezi hilo linatarajiwa kusindikizwa na maonesho ya vipaji vya kucheza kuimba na vinginevyo tofauti .
akizungumzia mutano huo ndugu Ibrahim kamwe "bigright" ambae pia ni kiongozi wa taasisi hiyo amesema, FOD au MARAFIKI WA MAENDELEO wamepanga kufanya uzinduzi wa mkutano wa dar es salaam ambapo ni makao makuu ya FOD iliyotapakaa karibu nchi nzima ikiwa na wanachama wengi,.
lengo la uzinduzi huo ni kuwatambulisha viongozi na kusajili wanachama wengine wengi zaidi na kuielezea FOD ilipo na inapokwenda.
aliongeza bigright kwa kusema FOD ina mikakati mingi kwa maendeleo ya vijana na taifa ila inakabiliwa na ukata mkubwa wa kujiendesha kutokana na uwa bado hawajapata mdhamini au mfadhili ambae angeweza kuisaidia hapa mwazo ambapo pagumu kwani ina mipango mingi ambayo hapo baadae itaweza kujiendesha kwa kuimarisha miradi yao.
baada ya mkutano huo wana FOD wanategemea kufanya shughuli za kijamii kwa kutembelea mahospitali mabarabarani na mashuleni kushiriki kuwasaidia kusafisha mazingira yao kwa kujitolea.
FOD wakati inahangaika kutafuta wadhamini pia inajipanga kuzunguka nchi nzima kutangaza USALAMA, AMANI NA UTULIVU hasa kipindi hiki cha tulicho nacho cha uchaguzi,
kwa kutumia mitandao ya kijamii,simu, sanaa za maigizo,michezo ,wanamuziki, na kuwakabili walengwa kwa maendeleo ya nchi yetu
MAWASILIANO NA WANA FOD
Ibrahim kamwe +255 713 501991
ibrakamwe@yahoo.com
au KATIBU WA FOD
JUMA NKWABI +255 715 527130
No comments:
Post a Comment