Pichani ni Mwenyekiti wa Kikundi cha Maigizo cha Kirumba Sanaa Group kilichopo Jijini Mwanza Katumba Khalid Maduwa akiwa na Kitambulisho chake cha Kupigia Kura.
Maduwa ambae pia ni Mshereheshaji (Mc Katumba) na Mtangazaji wa 99.4 Radio Metro Fm, ameungana na Binagi Media Group katika Kampeni yake ya Kuwahamasisha Watanzania waliojiandikisha katika daftari la wapiga kura kujitokeza kwa wingi katika kuwachagua viongozi bora wa kuwatumikia na si bora viongozi ambao wakati mwingine huchaguliwa kutokana na kutoa rushwa. Kampeni hiyo inaitwa "PIGA KURA, EPUKA KULA".
"Napenda kuwaasa Watanzania wenzangu kuwa tunahitaji uchaguzi wa Amani na Haki bila uvunjifu wa Amani. Tupige kura ili tuwachague viongozi sahihi kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa letu". Anasema Maduwa.
Bonyeza HAPA Kufahamu Zaidi.
No comments:
Post a Comment