ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 14, 2015

NAIBU WAZIRI WA MAJI MH. AMOS MAKALLA AKAGUA MRADI WA MAJI KATIKA MJI WA GEITA

Naibu waziri akikagua kazi za uchimbaji mitaro, ulazaji wa mabomba na ukaguzi wa tanki.
Mh Amos Makalla ( kulia ) akipewa maelekezo zaidi ya mradi huo


Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa akimpokea naibu waziri maji Amos Makalla.

Naibu waziri wa maji Amos Makalla leo ametembelea mradi  unaotekelezwa kwa ushirikiano wa serikali na mgodi wa dhahabu wa Geita(GGM) wa uboreshaji huduma ya maji kwa mji wa Geita
 
Mradi huu unagharimu fedha sh 10 bilioni ambao kukamilika kwake kutaongeza huduma ya upatikanaji maji kutoka asilimia 13 iliopo sasa hadi  kufikia asilimia 57
 
Kwa mujibu wa tathmini ya kazi iliyofanyika mradi huu unatarajiwa kukamilika  mwishoni mwa mwezi august mwaka huu na naibu waziri wa maji ameagiza wahakikishe wananchi wanapata maji wiki ya kwanza mwezi ya mwezi septemba na si vinginevyo

No comments: