Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (kushoto) akipata maelezo kuhusu na matumizi ya Gesi Asilia, Miradi na manufaa yake kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Bw. James Mataragio (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa Kongamano la Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora)
Waziri Membe akionyeshwa na Bw. Mataragio eneo bomba la gesi asilia
lilipopita kwenye Mchoro wa Ramani ya Tanzania uliopo mbele
yao.
Waziri Wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika
picha ya pamoja na Bibi Dorcas Membe (kushoto), Mtendaji Mkuu wa Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Bw. James Mataragio (Kulia),
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora, Bi Rosemary Jairo (wa pili kutoka
kulia) na Watumishi kutoka katika shirika
hilo.
Waziri Membe na Mkewe Mama Dorcas wakipata maelezo juu ya matumizi
ya radio calls kutoka kwa Bw. Sunji wa Kampuni ya Huawei
nchini alipotembelea banda la Kampuni ya hiyo wakati wa Kongamano la
Diaspora.
Waziri Membe (wa kwanza kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa
Afisa wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) nchini, Bi.
Matilda Nyallu. Kushoto kwa Mhe. Membe ni Balozi Mulamula, Katibu Mkuu
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Balozi Mulamula (katikati) akielezea jambo kwa Waziri Membe (kushoto).
Waziri Membe akisalimiana na mmoja wa Washiriki wa
Kongamano la Pili la Diaspora,Bw. William Malecela. Kulia ni Balozi
Mulamula na katikati ni Bi. Suzani Mzee kutoka Ofisi ya Waziri
Mkuu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Rosemary Jairo (wa pili
kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Itifaki, Bw. James Bwana (wa pili kutoka kushoto)na Maafisa
Mambo ya Nje Bw. Batholomeo Jungu ( kulia) na Bw. Amosi Tengu (
kushoto).
Picha na Reginald Philip
1 comment:
Mpeni mkurugenzi heshima yake ni doctor (PHD) sio bwana
Post a Comment