Advertisements

Friday, August 7, 2015

PICHA: WASANII WAMUAGA RAIS KIKWETE

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali (hawapo pichani),waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli,Dkt Jakaya Kikwete alizungumza mambo mbalimbali zikiwemo haki na hatimiliki za wasanii wa muziki pamoja na Bongomovie na pia alikubali kuwa mlezi wa tasnia hizo na kuhakikisha mambo yanakwenda sawa ndani ya tasnia hizo mbili adhimu kwa sasa hapa nchini.Picha na Ahmad Michuzi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete katikati pichani akiserebuka na wadau wa muziki na huku akipiga nao picha,ndani ya ukumbi wa Mlimani City  katika hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10 na pia kumtambulisha Mgombea wa Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akipiga ngoma huku akishirikiana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa ndani ya ukumbi wa mlimani City jijini Dar.
Mwanadada Wema Sepetu akimtunza midola Dkt John Magufuli alipokuwa akipiga ngoma jukwaani kwa ustadi mkubwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uuenezi Nape Nnauye na pamoja na Januari Makamba wakifurahia jambo kwa pamoja na wageni waalikwa mbalimbali waliofika ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameambatana na Mgombea Urais wa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli pamojoa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  (mwisho kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Paul Makonda wakiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City kushiriki hafla ya kuagwa kwake ilioandaliwa na Muungano wa Wasanii kwa ajili ya kumshukuru kwa namna alivyowasaidia tangu alivyoingia madarakani kwa miaka 10.
Rais Dr. Jakaya Kikwete akifurahia jambo  na Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kupitia CCM wakati alipowasili Mlimani City jijini Dar es salaam kwa ajili ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni kilichondaliwa na Muungano wa wasanii Kumshukuru Mh. Dr. Jakaya Kikwete kwa jinsi alivyowasaidia katika uongozi wake wa miaka 10 kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kumkaribisha Mgombea wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dr. John Pombe Magufuli, Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pia akishiriki tukio hilo.Hafla hiyo imehudhuriwa na wasanii mbalimbali  wakiwemo waigizaji wa filamu, wachezaji na wanamuziki wakishiriki kwa pamoja kumshukuru Dk.Jakaya Kikwete.
 Baadhi ya Wadau wa muziki wakifurahia jambo wakati Rais Dkt Jakaya Kikwete alipokuwa akiwasili ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na baadhi ya wadau wa muziki nchini ndani ya ukumbi wa mlimani City usiku huu.
 Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya Vodacom,Kelvin Twisa
 Dkt Kikwte akisalimiana na baadhi ya Wasanii wa muziki wa bongofleva
 Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick ndani ya ukumbi wa mlimani city usiku huu.
 Mmoja wa wasanii akiimba jukwaani kwa hisia.
Baadhi ya Wanamuziki wakongwe walihudhuria hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.









Wanauziki wakongwe pia walikuwepo kumshukuru Rais Kikwete kwa mambo mengi aliyoyafanya katika uongozi wake wa miaka kumi ndani ya tasnia ya muziki








 Mmoja wa wasanii akitumbuiza jukwaani usiku huu

No comments: