ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 16, 2015

POLISI MWANZA WATAWANYISHA UKAWA KWA MABOMU YA MACHOZI

Jeshi la polisi jiji Mwanza limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa vyama vinavyounda ukawa ili wasiandamane kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza kumpokea mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, anayetarajiwa kuwasili jijini huko kusaka wadhamini
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Charles mkumbo, amesema mabomu hayo yametumika ili kuwazuia wafuasi hao wasiweze kujazana uwanjani hapo na kusimamisha shughuli nyingine.

Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi

5 comments:

Unknown said...

ccm watanyooka tu.

Anonymous said...

polisi acheni unafiki hawa wananchi wangelikuwa wanakwenda kumpokea JK mngelivumbua utaratibu wa kuwalinda na kuweka usalama, na shughuli za wananchi wengine zingeli kwenda kama kawaida lakini hawa ni wapinzani wa serekali na serekali sio ya ccm ni ya wananchi lakini hilo jeshi letu la polisi hamku someshwa kule chuoni MOSHI sasa subirini huyu mheshimiwa wa monduli Lowassa atawaweka sawa mwaka huu.

Demokrasia sio ya chama kimoja ni ya vyama vingi kama watu hawakitaki chama chenu msiwan'gan'ganie ni vizuri mkakubali kukataliwa kwa hiari kuliko kukataliwa kwa nguvu wananchi wakichoka mabomu ya machozi sio dawa, hasa kwa kuwa nchi hii vilio ni jambo la kawaida kwa ajali zisizo kwisha na maisha yalivyo magumu.Msiogope upinzani huenda ikawa ndio suluhisho la matatizo ya jeshi lenu na nchi hii.

Anonymous said...

Mimi niko na swali dogo sana. Hivi hawa polisi ccm ikishindwa, watakula wapi??

Anonymous said...

CCM ikishindwa kitu hicho msahau. Vipi CCM ikishinda? Huyo fisadi mtaficha wapi?

Anonymous said...

Ccm cha moto mtakiona nyama nyie, mmezoea kuonea watu, sasa vumbi litatimka, na bado mnavyowapiga wananchi mabomu mtawatia hasira zaidi,, serikali ya Ccm inatafuta vita, na vitatokea, am just saying.