Advertisements

Monday, August 31, 2015

Presidential Debate

Hili ni suala la muhimu sana. Wananchi tunatamani sana tujue sera za wagombea uchaguzi wa rais kwa kinaga ubaga.Ni muhimu wote wapewe nafasi ya kutuelezea ya madhumuni yao kuwa rais wa Tanzania na ahazi zao kwa wananchi, sana sana katika masuala ya ufisadi, elimu , uchumi na maendeleo kwa ujumla.

Please kama unaweza kulirudia post ya Tarehe 8/30 kuhusu hili suala itakuwa vyema sana.

ASANTE SANA!

2 comments:

Anonymous said...

Hili lina umuhimu ni waTanzania wangapinwanaoweza kufuatilia kwa TV na wakati umeme wenyewe n unawashwa wakati wa Chama ya CCM ikiwa hewani na hata ukiwepo tutaona mabaya yakiandikwa kwa chama pinzani na mgombea wake ambao wanaonekana kuwa na nguvu. Angalia magazeti yanasema ubaya tuuu kwa yule mwenye nguvu ya upinzani mbona vyama viko vingi tuu na hatuoni wakisemwa. Swala ka ufisadi waulizwe CCM yenyewe na wagimbea wanaokalia ile swala la ESCROW na mh. Rais JK akalikimbatia. Madawa yankulevya na vipusa leo Mwakyembe anamsakama EL kutaka aonekane mbaya. Ukiwa waziri ulokamatavwatuhumiwa wengi tu pale aieport. Ilifunikwa kwa kuwa ilikuwa dili la viongozi na ukahamishwa idara. Kaja mhe Sitta na majuzi yakapita pembe kibao! Hiyo ni dili ya ufisadi inaendelea na hakuna majibu yeyote yaliyotolewa. Hizi hoja mnakija nazo.mpya za kuchafuana zinatoka wapi. Miradi iliyolala miaka kumi tunasikia inatolewa fedha kila mikutano huko mikoani. Huku wakisubiria kufungua mradi wa mabasi iliku iweka sera. Yaani imekuwa kazi ya kuwagilibu waTanzania tu.. Wanaolala na hali mgumu nankuamuka nayo kila siku iendayo kwa mungu. Hayo ndo.maisha bora kwa kila ..mhh.

Anonymous said...

Debate au mdahalo. Nani kasema Chama inayotawala inataka hilo. Huoni wanavyoandikwa mazuri ya uongo kwenye magazeti na Televisheni.!! Hawataki Demokrasia na ikiwepo ni kwamba analengwa mmoja tu. Hili hatulihitaji kwani haliko wazi kwa watanzania wengi. Tukomae hivyo hivyo hadi October 25 tujidamke. Acheni wizi wa kura na NEC iwe mkweli bila mapendeleo. Mwanasheria wa nchi hii tenda hali kwa waTanzania.