ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 13, 2015

Rais Kikwete Amzika Kisumo Mwanga


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kanisani wakati wa mazishi ya kada mkongwe wa CCM Mzee Peter Kisumo yaliyofanyika kijijini kwake Usangi-Mwanga Mkoani Kilimnjaro leo(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Mzee Peter Kisumo wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika huko kijijini kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifariji Mama Hosiana Kisumo Mke wa Marehemu Peter KJisumo wakati wa mazishi yake huko Usangi Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la Kada Mkongwe wa CCM Marehemu Peter Kisumo wakati wa mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake Usangi- Mwanga Mkoani Kilimanjaro leo.

2 comments:

Anonymous said...

Usahihi. Rais Kikwete hakumzika Peter K. Ila alishiriki maziko. Lugha gani hii mwandishi? Hata jeneza lenyewe hakuligusa kusaininkitabu na kutupa udongo kidogo angeshika chepe kama wengine. Acheni lugja za kupptosha. Yeye alishiriki maziko na sio kumzika. Walikuwepo viongozi wengine pia na wengine walinyimwa kutokana na ubabe wa kisiasa lakini kwa weli jinsi hii hakuna haki ya kumnyima mtu kiongozi au yeyote kushiriki. Mnona sote nkia ni mojah!!.

Anonymous said...

wewe anonymous wa 11:01am acha kupotosha watu. hakuna aliyenyimwa au kuzuiwa kwenda kuzika. lowasa alikuja na msafara wa mashabiki wake wa chadema,wakaambiwa msafara hauwezi kwenda ktk mazishi na bendera zao katika pikipiki na magari zitolewe. wenyewe wakaidi agizo la polisi na lowasa akaaamua kurudi moshi mjini. sasa nani kamnyima kushiriki mazishi???!!!!yeye lowasa anataka kuleta siasa katika mazishi ya familia za watu. amekosa uungwana kama mtanzania huwa hatufanyi tabia kama hizo. huyu mzee inaonekena yuko tayari kufanya lolote ili aingie ikulu. watanzania sio wajinga kiasi hiko