Nyie watu achene kufata mkumbo. Urais haujaribiwi. Eti tuwape miaka 5 Ukawa wakichemsha hatuwachagui tena!!! Ujinga gani huu Watanzania wenzangu? Tunajaribu kiti cha Urais. Hatuna uhakika na uchaguzi wetu tunatest zali!!! ONLY IN TZ.
Mara ooh Lowassa atadhibitiwa na viongozi mahiri wa Chadema/UKAWA!!! — nani pale unamuona anaweza kumwambia kitu Lowassa??? Mbowe? Mbatia? Lissu? Mnyika?? HAKUNA ATAEWEZA/ANAEWEZA KUMWAMBIA LOWASSA CHOCHOTE NDANI YA UKAWA. ATAFANYA ATACHOJISKIA, MSIDANGANYIKE. Huko ndo kawa Don kabisaaaa.
Jamani Magufuli anamaanisha anachosema. Kila alichokisema kwenye ufunguzi wa kampeni ndicho atachofanya. Amekuwa mtu wa hivi siku zote – kutekeleza asemayo. Yani unamuacha Magufuli unamchagua Lowassa!!! vichekesho hivi Watanzania wenzangu.
Huyo Lowassa tangu 1977 yupo ndani ya chama na ni kiongozi mkubwa tu tangu enzi hizo – ndani ya chama na serikalini. Leo atasemaje eti alikuwa hawezi kufanya mabadiliko yoyote? Kweli? Tena anayasema hayo baada ya kukatwa huku kwenye chama chake. Kwa nini asingejienguaga mapema huko nyuma akaonyesha hizo dalili zake za kutaka kuleta mabadiliko. Leo baada ya miaka 38 ndio anatuambia ngonjera hizi huku wote tukijua records zake za ufisadi. Maana ukiongelea uchafu wa serikali Lowassa huwezi kumuweka kando. Na mtu asiniambie sijui kama mnaushahidi mpelekeni mahakamani. Kila mtu anajua uozo wa katiba yetu na sharia zetu, huwezi kumpeleka mtu huyu kwa mfumo wetu wa sheria. Ila hakuna Mtanzania asiejua kuwa huyu ni JIZI, LIFISADI LILILOTUKUKA.
Halafu mtu ambae angesema kweli anaongoza mabadiliko tukaelewa alikuwa Dr Slaa peke yake. Huyu kweli unaona ana dhamira ya kweli na hii nchi. The rest ndani ya hicho chama hakuna kitu. Msipelekwe pelekwe jamani kama mang’ombe Watanzania wenzangu. Kuweni na reasoning. Haya, angalia hilo genge lao la UKAWA. Pale unaona nini kwa akili ya kawaida? Hata sie tusiojua siasa kivile tunaona genge la wapigaji na wenye uchu wa kuzidi kufilisi hii nchi wamejiunga pamoja. Jamani embu tusifate ushabiki. Tunajidharaulisha. Tuwe wakweli kwa nafsi zetu na kwa nchi yetu. Lowassa hafai kutuongoza. Na hawezi leo kutueleza chochote kuhusu mabadiliko kwani yeye ni mnufaika mkubwa wa mfumo dhalimu tunaoupigia kelele.
Leo atamsemaje JK wakati yeye ndio alikuwa anapita miji yote ya Tanzania kumuombea kura kabla hata ya kipenga cha ndani ya chama chao (2005)!! Watanzania nani ametufumba macho? Tunashindwa kuona ushenzi wa huyu mtu jamani!! Leo hii genge lao (Rostam na JK) lingekuwa kama zamani wala tusingemsikia anasema anataka sijui mabadiliko sijui anachukia umaskini. Tusingemskia. Halafu wenzangu niwaulize –unaiondoa CCM unamuweka Lowassa? Hahahhaha, Watanzania tunataka kufanya vichekecho. Tumshukuru Mungu kwa kuvunjika kwa genge lao (Rostam na JK) sasa Mungu ametupa mnyonge mwenzetu. Mwacheni Magufuli ashike dola na uenyekiti wa chama muone mambo yatavyoenda. MAGUFULI ANATOSHA NA ANAWEZA. Mungu atuongoze katika hili.
15 comments:
HUTUSHAWISHI KAMWE TUACHE NA LOWASA WETU
Huna Lako jambo Watanzania in wavivu wa kufikiri Kama alivyosema rais wenu mkapa
Lowassa yupo ukawa kwa masharti ya ukawa
Mbona wazungu wanaweza kuwa serikali ya umoja hata Zanzibar wamejaribu
CCM kwa unafiki
Naapa wanaweza na utakuwa mfano kwa Africa
Umepoteza mwelekeo na kama umechukua kidogodogo imekula kwako! Ahh basi baki ulivyotaka wewe. wewe Mageuzi yanaendelea.
Inaoneka bado sana hujaelewa maana ya siasa. You take things personal na pia hasira imetawala mawazo yako because your convincing power is poor. Unatukana watu na kuwaita wajinga. Siasa au democrasia sio matusi. What you wrote is your personal opinion. It is not scientific theory. Mawazo yako siyo facts because you can't prove scientifically that ukawa will fail the country. Maana ya kuwa na elimu ni kutoa mawazo yako wakati ukiheshimu mawazo ya watu wengine, na siyo kuwatukana unaotofautiana nao. Toa maoni yako ukishawishi watu wakubaliane na wewe. Na wale usiyokubaliana nao, siyo wajinga kwa vile wewe unajiona mwerevu. Heshimu mawazo yao. That is critical way of thinking.
Amina.
Nini sasa ulichoandika wewe mwandishi wa hii article?inabidi urudi shule haraka upeo wako ni mdogo sana,ata kama unatofautiana na mpinzani wako lazima uwe na legitimate point za kuandika.
Well said. Watanzania hatudanganyiki. Wamejaribu urais kupitia Chama tawala wakakatwa, katika week moja tayari wamebadilika na kuwa na uchungu na nchi. UKAWA wanalijua hilo, nambari one kwenye list of shame kulikuwa na jina hili. Chama kimefanya maamuzi magumu, kinara kaanguka sasa ana uchungu sana na nchi ataweza kuyafanya ambayo hakuyafanya miaka mingi sana. Kwa hili UKAWA wamehadaika na tamaa zao za madaraka (na fedha za kifisadi) na sio Mageuzi ya kweli, kila mtu ana haki ya kusema mawazo yake na kwa hili tutaendelea kusema hii siyo ile ya UKAWA ya Katiba, msitupige changa la macho na ulaghai ikulu si mahala pa usanii.
Wanaokushauri urudi shule wewe mwandishi wa hii article wanakupenda sana. Yani una bahati sana kupata ushauri mzuri kama huo. Itabidi utoe article nyingine kuwashukuru.
Mwandishi wa hii makala kama ungekuwa unakula vyakula vinavyoongeza aibu mwilini, usingekurupuka kuandika ulichokiandika. Hata hivyo tunaheshimu mawazo yako na ndo maana ya demokrasia.
Well blogger wetu ni CCM...but ccm for the past 39 yrs what have they achieved is graded zero so why waste bother 5 yrs for same waste.
Its time tupate change 4 real.
OMG, wewe mwenyewe mbona hakuna ulichoandika hapa. What kind of school did you attend? It must be an unaccredited Indian school!
Waswahili walisema "Mtaongea mchana na usiku mtalala". Kwa mantiki hii mchana ni sawa na wakati huu tunaoelekea kwenye uchaguzi na hivyo mengi yatasemwa. Baada ya uchaguzi usiku utaigubika Tanzania yetu wakati tutakapolala tukingojea matokeo ya uchaguzi. Mchana utarudi tena kwa wengi wakati matokeo yatakapo tangazwa. Watakaosherehekea ushindi mchana utaendelea kuwamulika na watakoshindwa giza litanda machoni mwao ikiwa ni ishara ya kutopata usafiri wa kuwapeleka walikotaka. Na haya yote mara nyingi yanamfanya mtu ajutie pale anapokuwa anasambaza sera ambazo lengo lake ni kuwazuga tu wanachi badala ya kuwaeleza ukweli ambao utasadia kuwachagua. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kuna kiongozi yeyote hapa duniani anaweza akatokomeza umasikini na kuwatajirisha wananchi wake wote au anaweza kutatua matatizo ya wananchi wake wote basi huyo kiongozi ni punguani. Hata hizi nchi zilizoendelea pamoja na majigambo yake yote bado matatizo yapo na masikini ni wengi pia. Wadau wenzangu tunaotoa changamoto zetu hapa mtandaoni lazima tuwe wakweli kuhusu kile tunachokiandika.
Naishi New York, Marekani, nchi inayofahamika kama imeendelea. Pamoja na yote haya kuna wananchi wengi tu ambao wanateseka wakiwa hawana kazi, mahali pa kulala na wengi hawajui hata watakula nini na wapi. Hii ndiyo nchi inayosemekana imebobea kwenye kidemokrasia na haki za binadamu. Ni nchi ambayo pia inatambulika kuwa ni tajiri. Kama ndivyo ilivyo katika nchi hii ni jambo gani atakalolifanya kiongozi wa nchi yetu kunyesha mvua ya mapesa yatakayomfanya kila Mtanzania kuwa tajiri? Hizi ni ndoto za alinacha sawa na hadithi za alfu lela ulela na hekaya za abunuasi tulizosoma kwenye vitabu. Tunakubali umasikini ni mbaya na hakuna anayetaka kuwa masikini, lakini ukweli ni kuwa tunaweza kupunguza makali na namba ya maskini lakini kuutokomeza kabisa sio swala la miaka mitano, kumi au hamsini kwani hakuna nchi yoyote duniani ambayo imefuta umaskini kabisa na kuwatajirisha raia wake wote. Hata Marekani na miaka yake zaidi ya 200 ya uhuru bado na kero la umaskini, ajira pungufu nakadhalika. Kwa nchi yetu sioni vipi mamluki hawa wanaojidai wanawajali sana wananchi hivi leo watawatolea janga hili kwa muda mfupi wakati wao wenyewe wamekuwa ni tatizo katika maendeleo ya nchi .
Mwalimu alisema maendeleo ya nchi yetu kama hayataletwa na CCM yanaweza yakaletwa na vyama vya upinzani vilivyotokana na kumeguka kwa CCM katika makundi mawili, wana CCM halisi ambao wangebaki ndani ya chama hicho na wana-CCM ambao walikuwa wanachama tu kwa vile hakukuwa na chama kingine ambao wangehama na kuanzisha chama cha upinzani. Mwalimu hakuimanisha kuwa mpinzani atabaki CCM zaidi ya miaka 10 tangia upinzani kuanzishwa ndiyo ahame. Huyu mtu siyo mpinzani bali ni mtu mwenye ajenda yake binafsi na hivyo tunatakiwa kumuogopa. Wapinzania walikuwa akina Dr. Slaa, Lipumba, Cheyo, Makani, Mtei na wengine aina hiyo ambao walihama CCM (kama walikuwa wanachama) na kuunda vyama vya upinzani mara tu kipenga cha kuanzisha vyama vya upinzani kupulizwa. Hawa wanaotoka CCM kwa ajili wameenguliwa ugombeaji kwa kukosa sifa na sasa wanaingia upinzani na wanajiita wanamageuzi hawana lolote wala chochote zaidi ya kupeleka vurugu kwenye vyama vtao vipya. Wakishindwa na huko wataishia kuviacha vyama hivyo solemba na kufanya upinzani nchini kupoteza nguvu zake zilizoanza kujijengea.
Tunajua upungufu wa chama tawala lakini tuna rekodi ya ufanisi wa kazi zake. Hatuna rekodi yoyote kutoka kwenye vyama vya upinzani zaidi ya majigambo ya kwenye majukwaa na sasa hii vurugu ya kwenye madaladala na sokoni kwa kujifanya ati wako karibu na wananchi. Tukumbuke kuwa hakuna majaribio katika kuongoza nchi hivyo lazima tuwe makini sana katika kuchagua viongozi wetu. Kumchagua kiongozi au chama ambacho huna uhakika au rekodi ya ufanisi wake kwa ajili tu unataka mageuzi ni hatari kwani ukifanya hivyo hakuna kurudi nyuma na matokeo yake yanaweza kuwa majuto. Kuondokana na wasiwasi wa matarajio yasiyokuwa na matumaini ni afadhali kuendana na msemo wa Waswahili kuwa “Zimwi likujualo halikuli likakumaliza”.
Watanzania watu twenye uvivu wa kila Kitu, uvivu wa akili, uvivu wa kujituma, uvivu wa kufikiri na ndio maana kwamba tayari wameshasahu kama lowasa alikuwa ccm na alikuwa na maskendo. Nasikia sisi watanzania tumekuwa wavivu hata wa kufanya matendo ya ndoa tunawaachia wakenya kuwashughulikia wadada wetu sasa hiyo ni hatari. Akili ya kutegemea kufanyiwa kila Kitu au kupata mafanikio kwa njia ya mkato(short cut ) ni asilimia 95% ya brain ya mtanzania. Lakini katika hali halisi ya maisha ni asilimia 5% peke yake mtu anaweza kufanikiwa kwa kutumia njia ya mkato sasa mimi sishangai kwa nini sisi watanzania tunabaki wamasikikni wakati wageni wanakuja wakiwa wao na nguo zao za mwilini lakini baada ya muda kidogo ndio wanaokuja kuwa matajiri wetu. Tunahitaji kiongozi atakae waongoza watanzania kwa vitendo kuwaondoa kuwa na mawazo tegemezi kwani katika nchi zilizoendelea wananchi ndio waliozoziendeza nchi zao serikali ni wasimamizi tu. Sasa nafikri Bwa magufuli ni msimamizi mzuri tu kupita wagombea wote wanawaowania uraisi kwa hivyo huyo ndio pekee wa kuchaguliwa utakapofika uchaguzi.
Blogger write about we cant take chance with UKAWA, why not? We took a chance with CCM for the past 50 plus yrs and we got nothing but more problems(the party of few, corruption, abusive, the rich ). Half of Tanzania is sold to foreigner because of the polices put forward by CCM government and it's leaders, the gape between rich and poor is even bigger than you can imagine , and Tanzania peoples are not benefit whatsoever by the richness of their country. All this is because of CCM. As a Tanzania I don't want to hear what CCM will do but Rutherford what they have done in past 20yrs
Blogger of August 26, 2015 at 4.06 AM. Thank you for your response to mine of August 25, 2015 at 7:14. I thought Swahili was the main language in this blog hence my using it. I have tried to reconstruct your English contribution thereby correcting few words that I thought were misplaced and looks like this:
Blogger *writes about *how we *can’t take chance with UKAWA, why not? We took a chance with CCM for the past 50 plus yrs and we got nothing but more problems (the party of few, corruption, abusive, the rich). Half of Tanzania is sold to *foreigners because of the *policies put forward by CCM government and *its leaders, the *gap between rich and poor is even bigger than you can imagine, and *Tanzanians are not *benefiting whatsoever *from the richness of their country. All this is because of CCM. As a *Tanzanian, I don't want to hear what CCM will do but *rather what they have done in *the past 20yrs
August 26, 2015 at 4:26 AM
On the subject matter I wrote that was purely my own opinion to the debate we are all contributing hoping that same will enlighten our fellow Tanzanians so that they can make informed decision when they go to the polls. You may agree or disagree with me and you have all the right to do so. For information, I personally have no grudges with opposition parties as well the ruling party itself. Actually, view multi party politics as a healthy political situation in any country. As indicated in my earlier my major concern is on the credibility of the opposition parties. By these parties accepting ex-ruling party members and giving them leadership roles while knowing that they are the same people they had in the past 10 years been accusing them of corruption, insensitive to peoples demands, enriching themselves, and what have you surely erodes the opposition parties credibility. If you rejected these people before and you now are embracing them how will the people see the difference between the opposition and the ruling party which you want to dethrone. Nevertheless, how can you convince the people that these newly found leaders are not there to just continue with the status quo they enjoyed from their old party? It is a shame but as I said earlier, this is my opinion, which you do not have to agree with.
Post a Comment