
Mnamo tarehe 10/08/2015
Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara
utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe. Lengo la
mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba wadhamini.
Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana
na Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo mbunge wa Mbeya Mjini
na baadhi ya Madiwani katika eneo la
Usalama wa Chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na
kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa
hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. hii inatokana na sababu za
kiusalama pia kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa
barabara kuu itakayotumika ni moja. Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya
miguu au pikipiki. Hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara
utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria
zitachukuliwa.
Imetolewa na:
Ahmed Z. Msangi – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.
7 comments:
Makubwa mwaka huu
Lakini ccm kweli Lowassa kiboko yenu
Magufuli alitembea na msafara wa magari toka mwanza Hadith Dar
Hivi nyie POLISI wa Tanzania mbona CCM wakiwa na mikutano yao hamtoi taarifa kama HIZI? Nyie mnapata shida ya mishahara na malazi kama sisi watanzania wengine. Je hamna uchungu kama sisi wengine kwamba CCM wamediriki kuifanya hii nchi na rasilimali zake kwamba ni za watu wachache? Hebu tuambiane ukweli. Jumba la Mkapa alilojenga huko Lushoto - YEYE NI TEMBO! Jumba la Kikwete huko Mboga au Chalinze YEYE analihitaji jumba lote hilo wakati majirani zake wote nyumba nyingi ni za NYASI? Jamani eehhhhh, tumefika mahali kama wananchi ambao tuliwapa dhamana ya KUONGOZA nchi yetu TUWAAMBIE - IMETOSHA! iMETOSHA NAPE, IMETOSHA KINANA, IMETOSHA JK, IMETOSHAAAAAA! Basi. Ondokeni kwa KURA, la sivyo msitupeleke sehemu mbaya! Mungu ibariki Tanzania. Mungu yabariki mabadiliko ya UONGOZI yanayokuja nchini mwetu! Amen
Je ni vyama vyote au tu kwa upunzani. Tutaona ya Chama tawala??!!
mbona mnatoa mapovu kabla ya oktoba, wewe aliyekwambia lowasa atashinda ni nani? lowasa mwenyewe analijua hilo ndio maana anatapatapa aonewe huruma, muulize ametoa wapi hela za kujenga nyumba ya billion tisa, ana heka 57,000 za ardhi. na ametoa wapi hela ya kumpa motto wake kuwa 60% ya mmiliki wa Vodacom. subiri kampeni zianze tumuache wazi na mjue ukawa mmechemka kudaka kaa la moto. povu bado hamjaliona nyinyi
Ya CCM tunayajuwa sana
Tunaichukia CCM Kama Hitler
hatuzungumzii la JK na RW 1 MWENYE MALI zilizotukuka nchi nzima je analipa kodi kiasi gani? nchi imetafunwa bado tunazidi kujiona tuko sawa. siku ya siku mtoto wako hataenda shule ndio ushabiki utaisha. WIZI kila kona hata mh. Raisi amelikubali na bado akashindwa kuwawajibisha kuna uhalali kweli hapa. ussife kamba shingoni.
Post a Comment