ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 13, 2015

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA KUHUSU MKUTANO WA CHADEMA

Mnamo tarehe 10/08/2015 Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba wadhamini.
Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo mbunge wa Mbeya Mjini na baadhi ya Madiwani katika eneo la Usalama wa Chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. hii inatokana na sababu za kiusalama pia kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja. Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki. Hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Imetolewa na: 
Ahmed Z. Msangi – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.

7 comments:

Anonymous said...

Makubwa mwaka huu

Anonymous said...

Lakini ccm kweli Lowassa kiboko yenu
Magufuli alitembea na msafara wa magari toka mwanza Hadith Dar

Anonymous said...

Hivi nyie POLISI wa Tanzania mbona CCM wakiwa na mikutano yao hamtoi taarifa kama HIZI? Nyie mnapata shida ya mishahara na malazi kama sisi watanzania wengine. Je hamna uchungu kama sisi wengine kwamba CCM wamediriki kuifanya hii nchi na rasilimali zake kwamba ni za watu wachache? Hebu tuambiane ukweli. Jumba la Mkapa alilojenga huko Lushoto - YEYE NI TEMBO! Jumba la Kikwete huko Mboga au Chalinze YEYE analihitaji jumba lote hilo wakati majirani zake wote nyumba nyingi ni za NYASI? Jamani eehhhhh, tumefika mahali kama wananchi ambao tuliwapa dhamana ya KUONGOZA nchi yetu TUWAAMBIE - IMETOSHA! iMETOSHA NAPE, IMETOSHA KINANA, IMETOSHA JK, IMETOSHAAAAAA! Basi. Ondokeni kwa KURA, la sivyo msitupeleke sehemu mbaya! Mungu ibariki Tanzania. Mungu yabariki mabadiliko ya UONGOZI yanayokuja nchini mwetu! Amen

Anonymous said...

Je ni vyama vyote au tu kwa upunzani. Tutaona ya Chama tawala??!!

Anonymous said...

mbona mnatoa mapovu kabla ya oktoba, wewe aliyekwambia lowasa atashinda ni nani? lowasa mwenyewe analijua hilo ndio maana anatapatapa aonewe huruma, muulize ametoa wapi hela za kujenga nyumba ya billion tisa, ana heka 57,000 za ardhi. na ametoa wapi hela ya kumpa motto wake kuwa 60% ya mmiliki wa Vodacom. subiri kampeni zianze tumuache wazi na mjue ukawa mmechemka kudaka kaa la moto. povu bado hamjaliona nyinyi

Anonymous said...

Ya CCM tunayajuwa sana
Tunaichukia CCM Kama Hitler

Anonymous said...

hatuzungumzii la JK na RW 1 MWENYE MALI zilizotukuka nchi nzima je analipa kodi kiasi gani? nchi imetafunwa bado tunazidi kujiona tuko sawa. siku ya siku mtoto wako hataenda shule ndio ushabiki utaisha. WIZI kila kona hata mh. Raisi amelikubali na bado akashindwa kuwawajibisha kuna uhalali kweli hapa. ussife kamba shingoni.