ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 12, 2015

Tofauti Kati ya Mrema na Lowasa Kwenye Ugombea Uraisi


Tofauti kati ya Mrema na Lowasa wote wakiwa wametokea CCM na wote wakiwa wagombea uraisi kupitia upinzani walikoingia bila kujua sera za vyama walivyoingia kwa kuwa waliingia chap chap ni kama ifuatavyo
1.Mrema alikuwa akiungwa na makundi ya wasomi waliobobea wakiwemo maprofesa walikuwa tayari kumbeba na kusukuma gari lake kuonyesha upendo wao kwake.Lowasa wasomi wamekaa naye mbali wengi hata kumsikia hawataki kuanzia wasomi wakubwa hadi wadogo.Slaa alikuwa kipenzi cha wasomi

2.Mrema aliungwa na watu wengi wa hali ya chini (walalahoi) ambao walimpenda bure bila gharama yeyote kwa kuwa alijitambulisha kama mlalahoi mwenzao wakawa wanamwunga mkono na kumsindikiza kwa makundi makubwa ya kutisha wakihemka kwa mihemko ya dhati ya kumwunga mkono mgombea wao.Lowasa haungwi mkono na walalahi wengi kwa kuwa kajitanabaisha kama mtu mwenye pesa anayetaka kumkomboa mlalahoi!! Walalahoi wazo la kukubali kuwa tajiri aweza kuwakomboa wengi wanalikataa hivyo Lowasa kumfanya akose waunga mkono kutoka kundi la walalahoi.Walalahoi wengine ambao wako tayari kumfuata ni wale ambao wanaamini kuwa Lowasa ana hela na wanataka pesa zake kwanza ili waandamane naye ana WAFUASI MASLAHI WENGI MNO ambao hawamwungi mkono kwa dhati kama ilivyokuwa kwa mrema.

3.Mrema alipoondoka CCM aliondoka na wafanyabiashara wengi wazawa kibao ambao walikuwa wakinyionyesha wazi na kumchangia hasa kwa ajili ya mbio za uraisi bila woga na kwa mapenzi ya dhati kwa mrema.Lowasa anaoondoka nao CCM ni watu maslahi si watu wenye hela wanaotaka kumsaidia bali wengi ni wale omba omba wavizia pesa za Lowasa wanaosubiri Lowasa atafute pesa awagawie!! Ziwasaidie ubunge,udiwani au katika mishe mishe za maisha yao.Ni watu wenye tamaa ambao wangependa wapenye waingie ndani ya Team lowasa kule kwenye fuko la hela hasa walibomoe.
Makundi ya wengi wanaohama CCM kumshabikia Lowasa ni wachovu kipesa na kimaisha wamepigika.Wanavizia LOWASA

4.Mrema alibebwa na vyombo vya habari bure hakutoa hata thumuni na misafara ya wasindikizaji ilikuwa ni ya bure hakuwapa chochote.Lowasa kuanzia vyombo vya habari visivyokuwa na haya kutwa vinawinda hela yake na wasindikizaji kuanzia bodaboda wanasema HAPENDWI MTU NI POCHI TU alete pochi tuingie barabarani.

5.Mrema alijipambanua kama mpiganaji wa wazi wa ufisadi Lowasa kauli mbio yake ni ya kuondoa CCM ,ufisadi ulimi wake unashindwa hata kutamka

Kwa ujumla Mrema alikuwa na nguvu kubwa kuliko Lowasa ya uungwaji mkono wa dhati.Kwa kuangalia aina ya waunga mkono Lowasa sisiti kusema uwezo wake wa kushinda Uraisi ni mdogo mno.Angekuwa na Sifa za mrema angalau angefurukuta.

Maoni Binafsi Kutoka Kwa YEHODAYA -JF

12 comments:

Anonymous said...

Huu uchambuzi hauna tofauti na wamtu aliyeishi zama za mawe, fikira duni ikiwa watu wote wanafikira kama hizi basi ni bora hata nikaombe uraia wa Somalia

Anonymous said...

NAPE AMEKULIPA KIASI GANI? HATA HIYO ANALYSIS NDOGO INAKUSHINDA.....MREMA HAKUJUA ANACHOFANYA NA ALIKUWA NA PAPARA. KWANINI UNAPOTEZA MUDA WAKO KUANDIKA USICHOKIFAHAMU?

Anonymous said...

CCM mnahangaika bure sana kujaza propaganda hapa
Hikii kimnauye na babu kinana wafunge midomo
Kwani watanzania 50% wenyeuwezo kwa kusoma mtandaoni na wote wasomi hatupendi CCM

Anonymous said...

Kabisa mrema alikuwa kiboko tuachane ushabiki wa kisiasa. Mtoa mada umeleta vitu vingi kuhusiana mrema ambavyo tulisha kuvisahau yule jamaa alikuwa moto wa kuotea kwa masafa lowasa cha mtoto. Analysis safi kabisa na huo ni ukweli halisi kwamba mrema alikuwa kiboko dhidi ya lowasa.mrema alikuwa mpigianaji wa kweli wa ufisadi . Lowasa /uroho wa madaraka zaidi hawana nia njema na nchi hii wanataka kuisambaratisha. Wapo tayari kuingia ikukulu kwa harama yeyote ile wakiongozwa na fisadi. Na wakishaingia kule basi watanzania hatuna nchi tumekwisha itakuwa majuto mjukuu. Tanzania ni ya watanzania wote sio ya watu wa sehemu fulani pekee yao.

Anonymous said...

Ushauri: Wananchi ni lazima tuwe makini sana na swala la Udini!! Hili ndilo adui mkubwa sana wa nchi yetu! Tusiwe tunakubali nchi yetu kuongozwa na viongozi wengi wa dini moja "dini dora" kama walivyoacha wakoloni! Hii ni kuitosa nchi yetu! Tuwe waangarifu sana na vyama vya siasa maslahi! Vyenye udini, ukabila na vyenye kukumbatia wenye pesa! Sisi wananchi wapiga kura ndiyo tunaoweza kuiokoa au kuitosa nchi yetu! Lakini kupanga ni kuchagua, tukichagua kuitosa nchi yetu hakuna jamii ya dini, kabila wala kundi la watu waliyolipwa pesa wataofaidika! Kitachotokea ni viongozi tuliyowashabikia kuondoka nchini na kutuachia vumbi!! Kuna msemo wa Kiswahili unaosema "Zimwi likujualo halikuli likakwisha!" Tutasikia mengi sana kwenye mchakato wa kampeni za urais, mengine ya kuvutia sana kutoka kwenye vyama dini, ukabila, upesa! Kuwa makini na kura yako!!!!

Anonymous said...

Habariiii ndio hiyo mada ya ukweli kabisa watu wanashabikia siasa kama team za mpira tu hamna jipya Magufuli oyeeee kandamiza mwana waneee.

Anonymous said...

Kwa kweli lowas ndo habari ya mjini zama za kale ni ccm tumeachana nayo mda sanaaaaa

Anonymous said...

Naipenda sana hii mada. Ukweli ni Kwamba Mrema hakujinunua kuingia upinzani. Lowasa kazimwaga bilioni 12 kuwahonga viongozi wa Ukawa wampitishe, and that's a FACT. Vile vile, Mrema aliunganisha na kujenga nguvu baina ya viongozi aliowakuta ambao wote walimpokea kwa shwari. Lowasa on the other hand, ameleta mpasuko Ukawa na kuwafanya Viongozi wawili mahiri kujitoa, am talking about Dr. Slås and Prof. Lipumba, Mrema aliwatia moyo wafuasi wa upinzani, lakini Lowasa ameingiza msukosuko unaowafanya wafuasi wengi wa Ukawa kutokuwa radhi, na wengi wapo tayari kuwafuata Lipumba na Slaa. Therefore, bila kuleta ushabiki wa chama chochote nadhani mada hii inachambua the pluses and negatives za ujio wa Lowasa kwenye upinzani na kama atawapa ushindi au ni dejavu !

Anonymous said...

YALE YALE, KILA ANAYEJUA KUANDIKA JAPO KIDOGO MADA YAKE NI ILE ILE,. JAMANI TUAMBIANENI YA MAGUFULI NA AHADI ZA LAPTOP KATIKA NCHI ISYO NA UMEME WALA MAJI? KWA KIFUPI TUANZE KUJADILI ISSUE, TUACHE KAZI RAHSI RAHISI ZA KUFANANISHA KILA TUNACHOKITIA MACHONI. MTOA MADA ANAZIDI KUONEHA UDHAIFU ULE ULE WA KUJADILI VITU AMBAVYO HANA TAKWIMU ZA KUTOSHA, ILHALI ANATUMIA MAJINA YA WATU KUPUNGA MAPEPO YA CHUKI NA HATIMAYE ANAJIKUTA ANATUMIWA NA WALIO NYUMA YA PICHA YA MAGUFULI. ANYWAY HIYO NI HAKI YA KINSINGI, ILA KUMBUKA KUENDELEA KULINGANISHA HATA WAKATI WALE MAJAMAA WALIOKUTAWALA MIAKA HAMSINI WATAKAPOTOKA NA KUSIMAMA MBELE YA PICHA YA MAGUFULI ,MAANA WAKATI HUO HAYA MAJAMAA HAYATAJALI KAMA WEWE NDIYE ULIKUWA MPAMBE WAO AMA LA. WAO NI KUKU-ESCROW, KUKU-EPA, KUKU-LOLIONDO,KUKU-RADAR.NA KUHAKIKISHA UKIUGUA HAKUNA DAWA, UKITAKA KUSOMA HAKUNA UMEME, UKITAKA PESA HAKUNA KAZI,..HABARI NDIO HIYO KUMBUKA IF I HAD KNOWN IS ALWAYS A SONG OF A FOOL!!

Anonymous said...

Comparison hizo juu, seems to be BEST-FIT, Why? Mada inaonyesha pambano la wagombea wawili wa kanda ya kaskazini. Mgombea wa zamani Mrema (Mchaga) VS Mgombea wa Ukawa (Mmasai, katika chama kilichojaa VIONGOZI Wachaga). Mada hii inawalinganisha hao wawili kwa sababu they have a lot in common. Both of them wanted/want to be the FIRST from Northern zone to become President of Tanzania. And, in fact, they both had/have the same sponsor/financier i.e. Mr. Mengi (Mchaga). Bwana Mengi amejaribu sana kwa miaka mingi, akitumia media/mitandao anayoimilikI ili kuhakikisha kama siyo Mchaga basi, somebody from that zone. Unfortunately, Mrema alishindwa kwa sababu hakupata kura kwenye mikoa ambayo iko very distrustful of Chagas (sorry). The same will apply to Lowasa, atapata Dar na mikoa ya kaskazini (Kilimanjaro, Arusha, Manyara} again, to the dismay of Mr. Mengi! The moral of this brief story ni kwamba: ACHENI UKABILA, kwani huwezi kuwa Rais kama mtaingiza ukabila, and that is the biggest shortcoming ya Ukawa/Chadema!.

Anonymous said...

Uchambuzi huu hauko vizuri. Umejengwa juu ya chuki dhahiri dhidi ya mtu. Na inaonekana kudhamiria kumpaka matope na kumharibia umaarufu.
Tuongee kwa takwimu kama kweli tumedhamiria kuijadili mada hii katika uhalisia.
Fuatilia uchukuaji wa fomu NEC
Kutafuta wadhamini Mbeya na
Leo hii Arusha.
Kwanini tunaandikia mate wakati wino tunao?
1995 upinzani ulikuwa na miaka 3 tu katika hali ya utitiri wa vyama vilivyojitenga
Leo hii umoja wa vyama vyenye nguvu
Mwamko wa upinzani ulikuwa mdogo sana 1995
Leo hii mwamko ni mkubwa
Hoja za ukabila, hoja za kutumia pesa bila kuwa na uthibitisho (evidence) tunahesabu kama ni majungu tu na chuki zisizo na sababu.
Lowasa ni msomi
Lowasa ana uzoefu
Lowasa anapendwa ndani na nje ya CCM
Lowasa anaaminiwa zaidi
Lowasa anajiamini

Unknown said...

Rudi shule kijana