ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 27, 2015

TUICO YAPATA VIONGOZI WAPYA MKOANI MBEYA

Katibu wa TUICO  Mkoa wa Mbeya Ndugu Merboth Kapinga akizungumza na wajumbe wa Tuico siku ya uchaguzi uliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Otu jijini Mbeya.(JAMIIMOJABLOG)
Wajumbe wa mkutano wakiimba wimbo wa pamoja.
Na Emanuel Madafa, Mbeya

CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri Mkoa wa Mbeya, kimefanikiwa kupata viongozi wapya watakao kiongoza chama hicho katika kipindi cha miaka mitano 2015  hadi 2020.



Uchaguzi umefanyika katika chuo cha wafanyakazi (Otu) jijini Mbeya na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka Taasisi za serikali na binafsi ambao wanawakilisha chama hicho cha (Tuico) mkoa wa Mbeya.



Akizungumzia uchaguzi huo, Katibu wa TUICO  Ndugu Merboth Kapinga, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za chama hicho ambacho zinaeleza kuwa kila baada ya miaka mitano ni lazima chama kichague viongozi wapya.



Amesema, wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.



Amesema, wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye vituo vyao vya kazi lakini matatizo hayo yanashindikana kutatuliwa kutokana na mambo madogomadogo ambayo yanahitaji kupatiwa ufumbuzi kwa pande zote mbili.



Hata hivyo amewataka viongozi hao kujenga uwezo wa kupambana na migogoro ya kifedha kwani ndio changamoto kubwa inayowakabili wafanyaazi na waajiri.



Aidha amesisitiza kuwa , wafanyakzi ni lazima wawajibike kwanza halafu ndio tudai haki nzetu kama vile nyongeza ya mshahara na motisha mbalimbali.



Viongozi hao waliopatikana ni Mwenyekiti wa chama hicho, Willium Mhando pamojana na wajumbe wa kamati tendaji, Boniface Mwanyamba kutoka kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi , Joyce Mwakifuna kutoka kampuni ya Coca Cola kwanza.



Wengine ni Mwanaidi Thadei na Michael Msovakumwao wajumbe kitengo cha biashara,  sekta ya fedha, Winifrida Kinyakisu na Mohamed Tangulia.

No comments: