Huu mdahalo unahitajika sana ili tuweze kuwajua vizuri hawa wanaotaka kuwa viongozi wetu. Wagombea wote wa vyama vinavyo shiriki wakutanishwe waulizwe maswali ya msingi (live) tuweze kupima majibu na uwezo wao. Midahalo ni imekuwa inapewa umuhimu mkubwa sana kwa nchi za wenzetu. Yawezekana kuna ambao wana sera nzuri lakini hatujapata nafasi ya kuwasikiliza. Uwezo wa kujieleza kwa kiongozi ni kitu muhimu sana. Pamoja na kwamba ahadi zinazo tolewa majukwaani huwa hazitimizwi zote, na hili siyo Tanzania tu bali hata nchi zilizo endelea; lakini pale mtu anapotamka anakuwa recorded. Mtu anaye kaa kimya ni ngumu kumwelewa na hutaweza kumhoji kwa kile ambacho hakutwambia au kuahidi.
MDAHALO UITISHWE
2 comments:
Hahaha nafikiri ndugu yangu huna history nzuri ya CCM ..CCM ni mwiko mgombea wao kuingia kwenye mdahalo..hilo halina mjadala:( ndiyo maana ni lazima tuwatoe hawa majambazi kama kweli tunahitaji demokrasia ya kweli Tanzania. .
Midahalo ipo uchaguzi wa mwaka huu. Subiri tutahabarishwa wakati muafaka ukifika.
Post a Comment